Pata taarifa kuu

Nchi za Afrika kuokoa raia wao nchini Ukraine

Nchi nyingi za Afrika, zikiwemo Nigeria na Afrika Kusini, zinajaribu kuwasaidia raia wao kukimbia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku kukiwa na ongezeko la shutuma za ubaguzi wa rangi dhidi ya Waafrika kwenye mpaka wa Ukraine.

Watu waliojitolea kutetea mji wao wa Kyiv, wakilinda barabara kuu inayoelekea Kiev.
Watu waliojitolea kutetea mji wao wa Kyiv, wakilinda barabara kuu inayoelekea Kiev. AFP - DANIEL LEAL
Matangazo ya kibiashara

Kama mamia ya maelfu ya watu, Waafrika wengi - wengi wao wakiwa wanafunzi - wanajaribu kutoroka Ukraine ili kuingia nchi jirani, hasa Poland.

Lakini shutuma za tabia ya ubaguzi wa rangi zinaongezeka na serikali ya Nigeria siku ya Jumatatu imezitaka mamlaka za forodha nchini Ukraine na nchi jirani kuwatendea haki raia wake.

"Kumekuwa na ripoti za kusikitisha (kwamba) polisi na maafisa wa usalama wa Ukraine wanakataa kuwaruhusu Wanigeria kupanda mabasi na treni" kwenda Poland, msemaji wa rais wa Nigeria Garba Shehu amesema.

"Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mama mmoja wa Nigeria akiwa na mtoto wake mchanga amelazimishwa kutoa nafasi alikokuwa ameketi kwa mtu mwingine," amebaini katika taarifa yake.

Bw Shehu amesema kuwa kulingana na ripoti zingine, maafisa wa Poland wamekataa raia wa Nigeria wanaotoka Ukraine kuingia nchini Poland.

"Ni muhimu kwamba kila mtu atendewe haki kwa heshima na bila upendeleo," amesisitiza.

Kundi la Waafrika Kusini, wengi wao wakiwa wanafunzi, wamekwama kwenye mpaka kati ya Ukraine na Poland, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini Clayson Monyela amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Balozi wa Afrika Kusini alizuru eneo hilo kujaribu kuwasaidia kuvuka mpaka, ameongeza Bw Monyela, ambaye alisema Jumapili kwamba Waafrika huko wanashikwa vibaya.

Raia wa Ukraine kwanza

Shutuma za ubaguzi wa rangi zimefutiliwa mbali hasa na balozi wa Poland nchini Nigeria, Joanna Tarnawska.

"Kila mtu anashughulikiwa sawa. Ninaweza kuwahakikishia kwamba kulingana na taarifa nilizonazo, baadhi ya raia wa Nigeria tayari wamevuka mpaka na kuingia Poland," ameviambia vyombo vya habari nchini Poland.

Kulingana na Bi Tarnawska, hati za utambulisho batili zinakubaliwa kuvuka mpaka na vizuizi vinavyohusiana na Covid-19 vimeondolewa. Raia wa Nigeria wana siku 15 kuondoka nchini, ameongeza.

Baadhi ya Wanigeria waliofaulu kuvuka mpaka walielezea safari zao kukabiliwa na hali ngumu kwenye mipaka iliyojaa watu ambapo maafisa walitoa kipaumbele kwa wanawake na watoto wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.