Pata taarifa kuu

Afrika yagawanyika katika azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine

Siku ya Jumatano, Machi 2, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha kwa wingi azimio la kutaka Urusi isitishe mara moja matumizi ya nguvu dhidi ya Ukraine. Nchi 141 ziliidhinisha nakala hii, 5 zilipinga na 35 zilijizuia. Zaidi ya nusu ya nchi hizi ni kutoka Afrika.

Matokeo ya kura ya Umoja wa Mataifa juu ya azimio kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Machi 2, 2022.
Matokeo ya kura ya Umoja wa Mataifa juu ya azimio kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Machi 2, 2022. © AP/Seth Wenig
Matangazo ya kibiashara

Nchi 28 za Afrika zimepiga kura kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa linalolaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Nchi moja (Eritrea) katika bara hiko imepiga kura ya kupinga azimio hilo. Na nchi 25 za Afrika zimejizuia kuegemea upande wowote. Nchi zilizopiga kura, lakini pia nchi ambazo hazikutuma wajumbe wao siku ya kupiga kura.

Afrika iliyogawanyika katika kambi mbili, amebaini Francis Kpatindé, mtaalamu wa masuala ya kisiasa huko Paris anaona kuwa: "Kwa upande mmoja, kuna nchi ambazo zinaweza kuelezewa kama zinaounga mkono nchi za Magharibi, nchi kama vile Nigeria, Côte d'Ivoire, Misri au Tunisia. Pamoja na Ghana, Gabon na Kenya, ambazo zote ni wanachama watatu wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Na kwa upande mwingine, kuna nchi, ambazo kihistoria zinazichukuliwa kuwa karibu na Umoja wa Kisovieti - miongoni mwa nchi zilizojizuia - kama vile Algeria, Angola, Congo-Brazzaville. Nchi ambazo zina mfumo wa kiutawala wa Marxism-Leninism. Na kuna marafiki wapya wa Urusi kama Jamhuri ya Afrika ya Kati. "

Kwa upande wa mtafiti huyu anasema, kujizuia kwa nchi hizinkunaelezewa kwa kiasi fulani kwa kurejea kwa sera ya kutofungamana na upande wowote ya miaka ya 1960 katika bara la Afrika, ikiongozwa na nchi kama Uganda, ambayo ndiyo kwanza imechukua uenyekiti wa nchi zenye sera ya kutofungamana, Tanzania au Afrika Kusini, ambayo baada ya kulaani uvamizi wa Urusi imerudi nyuma kuelekea sera ya kutoegemea upande wowote. Katika jukwaa la Umoja wa Mataifa, mwakilishi wa Afrika Kusini pia amesikitika kwamba azimio hili halikuweka mazingira mazuri zaidi ya mazungumzo na upatanishi.

Umbali fulani kutoka nchi za Kiafrika

Kuna tahadhari fulani ya kutojihusisha upande mmoja au mwingine katika mzozo ambao hauhusu moja kwa moja mataifa ya Afrika, amesema Profesa Mor Ndao, mwanahistoria wa Senegal: "Ni vigumu kuchukua msimamo kwa sababu Urusi imetoa mchango mkubwa. kusaidia vuguvugu la ukombozi wa taifa la Angola, Msumbiji, Guinea-Bissau, Cape Verde na Afrika Kusini. Na NATO na Jumuiya ya Magharibi zina mzozo fulani na Mataifa ya Kiafrika, hasa kwa mfano juu ya usimamizi wa mzozo wa Libya na athari zake katika siasa za kijiografia za Sahel barani Afrika. Kwa hivyo nadhani ni vipengele vyote hivi vinavyofanya mataifa ya Afrika kuwa mbali na mzozo huu. Ni msimamo wa busara unaowezesha hata Umoja wa Afrika kupeleka na kuwa mhusika katika masuala ya maridhiano na upatanishi. "

Lakini kujizuia kwa nchi za Afrika hakuwezi kuelezewa tu na nia ya kujilinda kutoegemea upande wowote dhidi ya kambi hizo mbili. Pia kuna nia ya kutoiudhi Urusi, mshirika mkubwa wa kibiashara na kijeshi katika bara hilo, ameongeza Michel Galy, profesa katika Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa huko Paris: "Kuna nchi ambazo ziko katika mchakato wa kupitisha ushirikiano na Moscow, iwe kupitia kundi la Wagner lililoingilia kati kama vile Mali au Jamhuri ya Afrika ya Kati. Na kisha, hivi majuzi kulikuwa na wajumbe kutoka Sudan kwenda Urusi ili kujenga upya ushirikiano wa kijeshi, hata kuanzisha kituo cha Urusi nchini Sudan. Kwa hivyo katikati ya mazungumzo, Sudan haina hamu ya kuitenga Urusi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.