Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Marekani kupiga marufuku uagizaji wa mafuta ya Urusi

Katika siku ya kumi na tatu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, usitishaji mapigano raia kutoka miji mbalimbali nchini Ukraine walikuwa wakisubiri kuhamishwa katika maeneo salama ya kiutu.

Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House huko Washington, Marekani, Februari 25, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House huko Washington, Marekani, Februari 25, 2022. © REUTERS / Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Huko Sumy, watu kadhaa waliweza kuhamishwa lakini kwa upande wa mji wa Mariupol, mamlaka za Urusi na Ukraine zinashtumiana kila upande kwa kutoheshimu usitishaji mapigano. Idadi ya wakimbizi wanaoondoka Ukraine imezidi milioni 2.

Ukraine imeanza Jumanne hii kuwahamisha raia kutoka mji wa kaskazini mashariki wa Sumy na kutoka mji wa Irpin ulioko karibu na mji mkuu Kyiv. Shughuli hiyo ya kuwahamisha watu imeanza baada ya maafisa wa Urusi na Ukraine kukubaliana kuunda maeneo salama ya kiutu ili kuwaruhusu raia kuondoka katika baadhi ya miji na maeneo yaliyozingirwa na wanajeshi wa Urusi.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Urusi Igor Konashenkov, amesema usitishaji mapigano umeanza asubuhi, na njia salaama zitafunguliwa kwa raia kutoka miji mikubwa ya Kyiv, Chernigov, Sumy, Kharkiv na Mariupol.

Kulingana na takwimu za hivi punde za Umoja wa Mataifa, watu 1,207 wamepata madhara tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuanza tarehe 24 Februari.

Idadi hiyo inajumuisha watu 406 waliouawa na 801 kujeruhiwa - lakini takwimu "zina uwezekano mkubwa kuwa idadi zaidi ya hiyo" anasema Liz Throssell, msemaji wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu.

Majeraha mengi ni matokeo ya "mashambulio ya anga na silaha za milipuko", unasema Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.