Pata taarifa kuu

Ukraine: Kundi la kwanza la raia wahamishwa huko Sumy

Katika siku ya kumi na tatu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, usitishaji mapigano raia kutoka miji mbalimbali nchini Ukraine walikuwa wakisubiri kuhamishwa katika maeneo salama. Huko Sumy, watu kadhaa waliweza kuhamishwa lakini kwa upande wa mji wa Mariupol, mamlaka za Urusi na Ukraine zinashtumiana kila upande kwa kutoheshimu usitishaji mapigano. Idadi ya wakimbizi wanaoondoka Ukraine imezidi milioni 2.

Afisa wa polisi wa Ukraine anakimbia huku akiwa amemshikilia mtoto baada ya mashambulizi ya mabomu katika mji wa Irpin, nje kidogo ya mji wa Kiev.
Afisa wa polisi wa Ukraine anakimbia huku akiwa amemshikilia mtoto baada ya mashambulizi ya mabomu katika mji wa Irpin, nje kidogo ya mji wa Kiev. AP - Emilio Morenatti
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Kulingana na shirika la Kimataifa la Nishati la Atomiki, kituo cha utafiti wa nyuklia kilipigwa na makombora ya Urusi karibu na mji wa Kharkiv.

► Siku ya Jumatatu Urusi ilitangaza kuanzishwa kwa "hatua ya kusitisha mapigano" na kupendekeza maeneo salama, ambayo raia watatumia kwa kukimblia. Kuhusu mji wa Sumy, ulioshambuliwa kwa bomu jana usiku, zoezi la kuhamisha raia limeanza. Lakini haiwezekani kwa wakati huu kujua kama hatu hii inaheshimishwa katika miji mingine ambayo zoezi hilo limepangwa kufanyika. Huko Mariupol, mamlaka inawashtaki kwa mara nyingine Urusi kwa kutoheshimu usitishaji wa mapigano.

► Idadi ya wakimbizi wanaoondoka Ukraine imezidi milioni 2, kulingana na UNHCR.

Wakati huo huo kulingana na vyanzo rasmi wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele kuelekea mji mkuu, Kiev.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.