Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Somalia: Amisom kubaili jina na kuwa ATMIS

Baada ya miezi kadhaa ya vizuizi, serikali ya Somalia na Umoja wa Afrika hatimaye wamekubaliana juu ya mageuzi ya Amisom ya sasa, ujumbe wa Umoja wa Afrika wa Kulinda Amani  nchini Somalia.

Kikosi cha wanajeshi wa Burundi walioko Somalia chini ya kivuli cha Amisom, mjini Mogadishu mnamo Julai 11, 2017.
Kikosi cha wanajeshi wa Burundi walioko Somalia chini ya kivuli cha Amisom, mjini Mogadishu mnamo Julai 11, 2017. © AFP / Mohamed Abdiwahad
Matangazo ya kibiashara

Amisom inatarajia kubadilisha jina lake na kuwa ATMIS, ikiwa na mamlaka ya kisiasa zaidi, na itakuwa na jukumu la kujiandaa kwa kuondoka kwa vikosi vya Umoja wa Afrika kutoka Somalia. Mamlaka hii mpya bado inahitaji kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Jina lililochaguliwa kwa ujumbe huu mpya, ujumbe wa mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), linapaswa kubadilishwa. Inalingana na kile ambacho mamlaka ya Somalia imekuwa ikidai kwa miezi kadhaa: kuchukua nafasi ya Amisom, ambayo imekuwepo kwa miaka kumi na tano na mapambano dhidi ya kundi la Al Shabab kama jukumu lake kuu, na kikosi chenye jukumu la kuitayarisha Somalia kuchukua majukumu yake ya usalama peke yake, ifikapo mwisho wa mwaka 2023.

ATMIS bado itabaki na kitengo chenye nguvu cha kijeshi huku nchi zinazochangia wanajeshi zikitarajiwa kubaki bila kubadilika.

Lakini kipengele cha kisiasa cha ujumbe huo kinapaswa kuimarishwa, kwa lengo la kusaidia Somalia kuleta utulivu katika taasisi zake na kuinua kiwango cha vikosi vyake usalama na jeshi. Na hii kuruhusu kuondoka hatua kwa hatua kwa wanajeshi wa Umoja wa Afrika bila kuhatarisha kwa kuweka ombwe la usalama hata kama wanamgambo wa Al-Shabaab wanaonekana kuimarika na wamekuwa wakiongeza mashambulizi yao kwa wiki kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.