Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Somalia: Mogadishu yalengwa na mashambulizi yanayodaiwa na Al Shabab

Milio ya risasi na milipuko ilisikika jana usiku huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. Haya ni mashambulizi yaliyotokea kwa wakati mmoja ambayo yalifanywa na kundi la wanajihadi la Al Shabab. Hasa, kituo cha polisi kililengwa na kuharibiwa.

Baadhi ya watu wakiwa karibu na jengo lililoharibiwa na bomu llililotegwa katika gari, Februari 16, 2022.
Baadhi ya watu wakiwa karibu na jengo lililoharibiwa na bomu llililotegwa katika gari, Februari 16, 2022. AFP - HASSAN ALI ELMI
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji walitimuliwa, lakini mashambulizi haya yanakuja wakati hali ya kisiasa nchini Somalia bado ni tete. Mbali na mzozo wa kisiasa na mchakato mgumu wa uchaguzi ambao nchi inapitia, wakazi wa Mogadishu wanakabiliwa na wasiwai mkubwa kutokana na machafuko yanayosababishwa na ugaidi.

Mogadishu yakumbwa na shambulio kubwa

Wakati wa usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, karibu saa saba, mji mkuu wa Somalia ulikumbwa na shambulio kubwa. Kundi la watu waliojihami kwa silaha za kivita waklifanya mashambulizi kwa wakati mmoja dhidi ya maeneo mawili ya kaskazini na kusini mwa jiji, Kahda na Dar-el-Salam.

Huko Kahda, gari lililokuwa limetegwa bomu lilielekezwa dhidi ya kituo cha polisi, ambacho kiliharibiwa kabisa, pamojana nyumba za raia karibu na eneo hilo, kulingana na picha zilizoto lewa Jumatano. Wakaazi wa vitongoji vyote viwili waliripoti mapigano makali ya silaha ndogo ndogo wakati wa usiku kwa takriban dakika 30, ambapo washambuliaji walikimbia.

Vurugu za kigaidi hazikomi

Siku ya Jumatano, hali ya utulivu imerejea. Na asubuhi ya leo, Al Shabab walidai kuhusika na mashambulizi haya, wakisema walikuwa wameshambulia maeneo sita tofauti katika mji mkuu. Polisi waliripoti vifo kadhaa, wakiwemo watoto. Lakini ripoti hii bado ni ya muda.

Ghasia za kigaidi hazikomi nchini Somalia. Mwezi mmoja uliopita, msemaji wa serikali alijeruhiwa katika shambulio la kujitolea mhanga. Kisha wiki moja baadaye, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua kwenye makutano ya jiji yenye shughuli nyingi, na kuua watu watatu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.