Pata taarifa kuu

Pembe ya Afrika: FAO yaonya juu ya msaada wa haraka ili kuepusha mgogoro wa chakula

Pembe ya Afrika iko katika hatari ya kupitia mojawapo ya migogoro mibaya zaidi ya chakula duniani, limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO).

Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea (picha ya kielelezo).
Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea (picha ya kielelezo). © AP Photo/Elias Meseret
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Covid-19 na miaka miwili mfululizo ya uvamizi wa nzige, wakazi wa vijijini wanakabiliwa na msimu wa tatu wa ukame kutokana na Niña, jina ambalo limetolewa kwa kiwango kikubwa cha joto la baharini kando ya Bahari ya Pasifiki ya kati.

Nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, hasa, zaidi ya watu milioni 25 wako katika hatari ya kuwa na uhaba mkubwa wa chakula ifikapo katikati ya 2022. Wakulima milioni 1.5 na wafugaji ni miongoni mwa waliodhoofishwa zaidi na ukame huo,  ambao wanahitaji msaada wa dharura ili kupitia msimu huu wa usio kuwa wakawaida, kama ilivyoelezwa na Rodrigue Vinet, msemaji wa FAO.

Ni vizuri kufahamu kwamba ng'ombe akifa, mara moja husababisha watoto wawili kukosa tena bakuli lao la kila siku la maziwa. […] Ni lazima tuchukue hatua, kwa lazima na mara moja, mnamo mwezi huu wa Januari, Februari na Machi. Baada ya hapo, kwa bahati mbaya, itakuwa imechelewa sana.

Wakati wa mgogoro wa awali wa chakula katika Pembe ya Afrika, mwaka 2017, jumuiya ya kimataifa iliichukuwa hatua haraka, wakati mwaka 2011 ilijibu kwa kuchelewa. Watu 260,000 walifariki dunia kwa njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.