Pata taarifa kuu
SOMALIA

Watu sita wauawa mjini Mogadishu baada ya shambulizi la bomu

Watu sita wameuawa mjini Mogadishu nchini Somalia, baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu nje ya mkahawa, karibu na kizuizi cha kukagua magari, kwenye barabara ya kuelekea katika makaazi ya rais.

Shambulizi la bomu mjini Mogadishu nchini Somalia
Shambulizi la bomu mjini Mogadishu nchini Somalia © REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa usalama mjini Mogadishu amesema, wakati wa mlipuko huo, êneo hilo lilikuwa na watu wengi, na waliopoteza maisha ni raia wa kawaida, huku wengine  12 wakijeruhiwa.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini waliohusika na mlipuko huo, lakini walioshuhudia wanasema aliyerusha bomu hilo, alikuwa mlipuaji wa kujitoa mhanga.

Mji wa Mogadishu umeendelea kushuhudia mashambulizi kama haya katika siku za hivi karibuni, katika taifa hilo ambalo linaendelea kushuhudia changamoto za kiusalama na siasa, baada ya vongozi kutofautiana kuhusu kufanyika kwa uchaguzi.

Kucheleweshwa kufanyika kwa uchaguzi huo, kunawapa mashaka washirika wa kimataifa wan chi hiyo ambao wanaona, kunatoa mwanya kwa makundi ya Al Shabab na Al Qaeda kuendelea kuwa tishio kwa serikali.

Marekani imetangaza hatua ya kuwanyima vibali vya kusafiria, watu wanaokwamisha mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.