Pata taarifa kuu

CAR: Mnyarwanda Valentine Rugwabiza achukua usukani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa

Alikuwa ameombwa kugombea nafasi hiyo kwa wiki kadhaa, hatimaye amechukuwa nafasi ya mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jmhuri ya Afrika ya Kati, Minusca.

Valentine Rugwabiza, Mkuu mpya wa Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Valentine Rugwabiza, Mkuu mpya wa Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. AFP - GEORGES GOBET
Matangazo ya kibiashara

Mnyarwanda Valentine Rugwabiza atachukua nafasi ya Mankeur Ndiaye kutoka Senegal kama mkuu wa Minusca, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tangazo hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres usiku wa kuamkia siku ya Alhamisi kutoka New York. Ni mwanadiplomasia wa muda mrefu ambaye anachukua hatamu ya uongozi wa Minusca.

Tangu mwaka 2016, Valentine Rugwabiza amekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa. Waziri wa zamani wa Paul Kagame, Mkuu wa Baraza la Maendeleo la Rwanda, naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani, mwanadiplomasia huyo mwenye umri wa miaka 59 tayari ameonesha kuwa ni mchapa kazi kwa kiasi kikubwa.

Mamlaka ya Mankeur Ndiaye itakamilika Februari 28. Anaondoka madarakani "bila majuto", kulingana na wale walio karibu naye, baada ya zaidi ya miaka mitatu yenye misukosuko katika uongozi wa Minusca. Mwanadiplomasia huyo wa Senegal kwenye twitter amemtakia mrithi wake "mafanikio kamili na bahati njema".

Mfululizo huu unakuja wakati mahusiano yanadorora hasa kati ya Bangui na Minsuca, ambapo askari wake wanne walizuiliwa na polisi kabla ya kuachiliwa siku ya Alhamisi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alihimisha askari hao waachiliwe mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.