Pata taarifa kuu

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wamalizika kwa mtafaruku mkubwa

Wakati mapigano yakiendelea kaskazini mwa Ethiopia, na hasa katika eneo la Afar, wakuu wa nchi za Afrika walikusanyika katika mji mkuu Addis Ababa kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mwishoni mwa juma hili.

Moussa Faki Mahamat (Mwenyekiti wa Tume ya AU), Macky Sall (Mwenyekiti wa AU) na Leslie Richer (Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tume) mnamo Februari 6, 2022 huko Addis Ababa.
Moussa Faki Mahamat (Mwenyekiti wa Tume ya AU), Macky Sall (Mwenyekiti wa AU) na Leslie Richer (Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Tume) mnamo Februari 6, 2022 huko Addis Ababa. REUTERS - TIKSA NEGERI
Matangazo ya kibiashara

AU imekuwa ikifanya kazi kwa miezi kadhaa kutatua mzozo wa Tigray. Majaribio haya hadi sasa hayajafaulu. Umoja huo unahakikisha kuwa utaongeza juhudi zake ili kupata usitishaji vita.

Rais wa Senegal Macky Sall, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa  AU ameuomba Umoja wa Afrika kupitisha azimio "kali" zaidi, na "ngumu". Senegal Macky amebaini kwamba umoja huo lazima uunge mkono bila shaka vikwazo vilivyochukuliwa na ECOWAS dhidi ya Mali, hasa, ameripoti mwandishi wetu maalum huko Addis Ababa, Florence Morice.

Kamwe katika historia ya taasisi hiyo nchi nne hazijwahi kusimamishwa katika AU katika kipindi cha miezi kumi na miwili. "Hali hiyo inatoa hisia kwamba Afŕika imerejea katika miaka ya 1970,” amelaumu Moussa Faki Mahamat, ŕais wa Tume ya Umoja wa Afrika. Changamoto inayoikabili taasisi hii leo ni kuimarisha uwezo wake wa kuzuia maambukizi haya.

Kuhusu suala lenye utata la hadhi ya waangalizi iliyotolewa kwa Israel mwaka jana, wakuu wa nchi za Afrika hawakuweza kukubaliana. Kwa hiyo walichagua kukabidhi swali hilo kwa kamati ya wakuu sita wa nchi, wenye jukumu la kutafuta mwafaka… badala ya kupiga kura na kueneza mifarakano yao.

Kushindwa kwa upatanishi wa amani nchini Ethiopia

Kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ethiopia, nchi mwenyeji wa mkutano huo, haikutajwa wakati wa hotuba za kuhitimisha, amesema Noé Hochet-Bodin, mwandishi wetu mjini Addis Ababa. AU imekuwa ikifanya kazi kwa miezi kadhaa kutatua mzozo wa Tigray. Majaribio haya hadi sasa hayajafaulu.AU imehakikisha kwamba itaongeza juhudi zake ili kupata usitishaji mapigano.

AU ilimteua mjumbe wake maalum wa Pembe ya Afrika mnamo mwezi Agosti 2021, karibu mwaka mmoja baada ya mapigano kuanza kaskazini mwa Ethiopia. Tangu wakati huo, ziara mbalimbali za Olusegun Obasanjo kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray zimesalia bila mafanikio, na pande zote mbili zinapuuzia wito wa amani.

Jumapili hii, Tume ya Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika ulijitetea kutokana na uzembe na kutochukua hatua yoyote. "Tumekuwa tukishughulikia shida hii tangu siku ya kwanza. Tumesisitiza tena hitaji la kutafuta suluhu la kisiasa ambalo limejikita katika mchakato wa maridhiano ya kitaifa na mazungumzo, hasa kwa kutumwa kwa wajumbe watatu Addis Ababa mwanzoni mwa uhasama, " alitangaza Kamishna Bankole Adeoye. mnamo Novemba 2020. wakati huo wajumbe watatu walifukuzwa kazi mara moja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Olusegun Obasanjo atasafiri tena wiki hii hadi Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.