Pata taarifa kuu
BENIN-USALAMA

Benin: Wanane wafariki katika makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa dhehebu moja

Makabiliano ya Jumamosi Januari 29 kati ya polisi na wafuasi wa Kanisa la Azael, linalotajwa kuwa dhehebu, yalisababisha vifo vya watu wanane katika wilaya ya Monkpa, wilaya ya mji wa Savalou, katikati mwa nchi. Maafisa wawili wa polisi ni miongoni mwa waliofariki. Mchungaji na wafuasi wake kadhaa wako mafichoni.

Wilaya ya mji wa Savalou, katikati mwa nchi.
Wilaya ya mji wa Savalou, katikati mwa nchi. © Wikimedia Commons CC BY SA 4.0 Tchokponhoue josué
Matangazo ya kibiashara

Maafisa hao wawili wa polisi walitekwa nyara kwanza kabla ya kuuawa na waumini wa Kanisa lililoitwa Azael. Mwanzilishi ni kijana wa Benin kutoka Nigeria, hakuna mtu anayeweza kuainisha harakati zake kwa sababu ya imani yake. Kanisa lao limejengwa katikati ya kichaka, wafuasi wamepigwa marufuku kukata nywele zao.

Mwanzilishi, anayechukuliwa kuwa mkuu wa dhehebu hilo, amekuwa akihutubia waumini wake kuwa mwisho wa dunia umefika na kupendekeza kila mtu auze bidhaa zake. Ni kwa jina la kauli mbiu hii ambapo kundi lake limekuwa likivamia mazao ya wakulima kwa jeuri.

"Mchungaji" anayetafutwa sana

Polisi walipokea malalamiko kadhaa kutoka kwa wakulima, dhidi ya mwanzilishi wa dini hii, lakini hakuweza kuripoti. Siku ya Jumamosi maafisa wa usalama walikwenda katika makao makuu ya kanisa hilo, lakini walikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wafuasi wa kanisa. Maafisa wa polisi walilazimika kufyatua risasi hewani wakijaribu kuzuia wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini kuchoma kituo cha polisi.

Idadi ya watu wanane waliofariki katika makabiliano hayo, waumini sita na maafisa wawili wa polisi, ilisambaa siku nzima ya Jumamosi. Mtu mashuhuri katika eneo hilo ameripoti kifo cha mtu wa saba ambacho hakijathibitishwa na mamlaka. Jeshi lilikwenda kusaidia vikosi vya salama, lakini hali imedhibitiwa kulingana na polisi. Mchungaji huyo yuko mafichoni na anatafutwa udi na uvumba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.