Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Sintofahamu yajitokeza kuhusiana na kutoroka kwa wavuvi wa Niger wanaoishi Benin

Mamalaka nchini Niger inadai iwapo wavuvi wa Nigeria, waliokuwa wakiishi karibu na mipaka ya Benin na Burkina Faso, walilazimishwa kurejea nchini mwao baada ya shambulio la wanajihadi dhidi ya ngome ya kijeshi nchini Benin huko Porga mapema mwezi Desemba? Lakini kwa upande wa Benin, inaaminika kuwa si sahihi kuzungumza juu ya kuondoka kwa lazima au kufukuzwa. Familia hizi zinasemekana kuondoka kijiji cha Kualou kwa hiari yao.

Wanajeshi wa Niger wakishika doria kati ya Agadez na Arlit
Wanajeshi wa Niger wakishika doria kati ya Agadez na Arlit ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamia kadhaa ya wavuvi wa Niger, pamoja na wanawake na watoto, wamerejea katika vijiji vyao vya asili katika maeneo ya vijijini ya Gatwani na Tounouga, katika wilaya ya Gaya, inayopakana na Benin, ameripoti Moussa Kaka, mwandishi wetu wa Niamey.

Kwa mujibu wa mamlaka ya Niger, ambayo inathibitisha taarifa hizo, wavuvi hao, ambao baadhi yao wameishi katika sehemu ya Benin kwa zaidi ya miaka thelathini, wametakiwa kurejea katika nchi yao ya asili.

Kurudi huko kwa kulazimishwa ni kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya ngome ya jeshi la Benin huko Porga Desemba 2. Kulingana na vyanzo kadhaa, vikosi vya Benin vinafanya kazi katika eneo hili la mpaka kati ya Benin na Burkina Faso, na uwepo wowote wa raia katika eneo hili la vita, ambapo wanajihadi wanaweza kujificha kwenye vitongoji, sio jambo la kuhitajika.

Kulingana na watu wa kwanza waliowasili katika kijiji chao cha Gatwani nchini Niger, zaidi ya watu 500 wamekimbia kijiji cha Kualou, kwenye mpaka kati ya Benin na Burkina Faso. "Niger imefanya mipango yote ya kuwakaribisha raia wake," amesema gavana wa eneo la Dosso. Msaada mkubwa wa chakula ulisambazwa kwa kaya 81 zilizofukuzwa kutoka Benin na kurudi bila mizigo wowote. Wengi wamelalamika kuwa wametelekeza mashamba yao ya mpunga na mihogo bila mavuno. Suala hili linapaswa kushughulikiwa kwa njia za kidiplomasia.

"Hatukufukuza mtu yeyote"

Hata hivyo, Benin inatoa toleo lingine la kihistoria,amesema Jean-Luc Aplogan, mwandishi wa RFI huko Cotonou. "Hatujamfukuza mtu yeyote," amesema mmoja wa maafisa wachache wa Benin ambao wamekubali kuzungumzia suala hilo. Hakuna maoni au taarifa kwa vyombo vya habari kwa sasa. Serikali ya Benin iko likizoni, amesema waziri mmoja.

Kilomita 6 kutoka Kualou, mji ambao mamia ya wavuvi walikimbia, mkuu wa kijiji cha Porga, Pierre Yani Wandja, akihojiwa kwa njia ya simu, amesema alijionea mwenyewe kundi la kwanza likiondoka saa chache baada ya shambulio la Desemba 2. Anadhani kuwa wavuvi wa Niger waliondoka kwa "hofu ya magaidi na kupituliwana risasi hewa".

Kulingana na habari zetu, wahusika wa shambulio la Desemba 2 waliwasili kwa mitumbwi. Mara baada ya kuwasili eeneo la tukio, jeshi la Benin liliharibu mitumbwi, kulingana na duru za kuaminika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.