Pata taarifa kuu
BENIN-HAKI

Benin: Mpinzani Reckya Madougou ahukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela

Uamuzi huo umetolewa alfajiri, Jumamosi hii, Desemba 11: mwanasiasa wa upinzani wa Benin na Waziri wa zamani wa Sheria, Reckya Madougou, kuroka chama cha Democrats, amehukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela na kutakiwa kulipa faini ya faranga za CFA Milioni 50.

Wafuasi wa Reckya Madougou mbele ya mahakama huko Porto-Novo.
Wafuasi wa Reckya Madougou mbele ya mahakama huko Porto-Novo. Yanick Folly AFP
Matangazo ya kibiashara

Washtakiwa wengine watatu pia wamehukumiwa kifungo hicho na wengine wameachiliwa. "Sijawahi kuwa na sitakuwa gaidi," amesema Reckya Madougou, muda mfupi kabla ya kutangazwa kwa hukumu yake.

Reckya Madougou alitumia karibu saa 24 akiwa kizimbani kabla ya kujua hatima yake. Reckya Madougou amehukumiwa kifungo cha miaka ishirini jela na kutakiwa kulipa faini ya faranga za CFA Milioni hamsini. Washtakiwa watatu kati ya watano wamepewa hukumu kama hiyo. Wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo, Bi. Madougou, akiwa amesimama huku akiwa amefumbatia mikono yake, alionekana mdhaifu.

"Ninajitolea kutetea demokrasia"

Dakika chache kabla, wakati jaji mkuu alipomuuliza kama ana lolote la kuongeza katika utetezi wake, alikuwa na hitimisho hili: “Leo ninajitolea kwa ajili ya demokrasia. Ikiwa hii itawawezesha majaji wa mahakama hii kupata tena uhuru wao basi nisingepatwa na masaibu haya bila sababu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.