Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika wataka kuzindua upya mazungumzo kati ya Mali na ECOWAS

Ujumbe kutoka Umoja wa Afrika ulikuwa mjini Bamako Jumanne tarehe 25 Januari. Mwenyekiti wa Tume ya AU, Moussa Faki Mahamat, alikutana na mamlaka ya mpito. Alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje Abdoulaye Diop, Waziri Mkuu Choguel Maïga na Rais wa Mpito, Kanali Assimi Goïta.

Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, Desemba 18, 2018 wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Austria.
Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, Desemba 18, 2018 wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna, Austria. AP - Ronald Zak
Matangazo ya kibiashara

Iwe kwa upande wa wajumbe wa Umoja wa Afrika au mamlaka ya mpito ya Mali, hawakutaka kuleza kuhusu maudhui ya mazungumzo yao. "Alikuja kusikiliza tu, kuelewa jinsi ya kuzindua upya mazungumzo", amesema mshauri wa Waziri Mkuu, baada ya mahojiano kati ya Choguel Maïga na Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Ulikuwa ni mkutano katika mfumo wa kukutana tena kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop, ambaye alikuwa bado, hadi mwezi Machi mwaka uliyopita, mkurugenzi katika ofisi ya Moussa Faki Mahamat. Wadhifa ambao alikuwa amejiuzulu kwa sababu za kibinafsi kabla ya kujiunga na serikali ya mpito miezi michache baadaye.

Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Mali, rais wa Tume ya Umoja wa Afrika aliomba "mbinu ya maelewano ambayo inaweza kutunza maslahi ya kimsingi" ya Mali, "kulingana na sheria za" ECOWAS na Umoja wa Afrika.

Tangu Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ilipoweka vikwazo vyake, zaidi ya wiki mbili zilizopita, licha ya matamko ya uwazi wa mazungumzo, bado kunaripotiwa pambano kati ya jumuiya hiyo ya kikanda na Bamako. Algeria ilipendekeza upatanishi wake na kupendekeza ratiba fupi ya kuandaa uchaguzi na kurejea kwa utaratibu wa kikatiba: kipindi cha miezi kumi na sita dhidi ya miaka mitano kisha minne iliyopendekezwa hapo awali na Bamako. Hoja hii ya Algeria inaungwa mkono na Umoja wa Afrika, AU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.