Pata taarifa kuu
MALI-VIKWAZO

Mali: Viongozi wa mapinduzi waitisha maandamano dhidi ya vikwazo

Kwa wito wa viongozi wa mapinduzi nchini Mali, maandamano makubwa yamepangwa kufanyika Ijumaa hii, Januari 14 katika mji mkuu wa Mali. Maandamano hayo yataanzia katika eneo la Uhuru.

Kwa wito wa viongozi wa mapinduzi nchini Mali, maandamano makubwa yamepangwa Ijumaa hii katika mji mkuu wa Mali, eneo la Uhuru.
Kwa wito wa viongozi wa mapinduzi nchini Mali, maandamano makubwa yamepangwa Ijumaa hii katika mji mkuu wa Mali, eneo la Uhuru. AFP - MICHELE CATTANI
Matangazo ya kibiashara

Lengo la maandamano haya ni kushutumu vikwazo dhidi ya Mali vilivyochukuliwa katika mkutano wa mwisho wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS. Hatua kadhaa zimepangwa wakati wa mkutano huu katika mji mkuu wa Mali.

Wanasiasa wengi, viongozi wa vyama, na vuguvugu za vijana au hata wananchi, wanatarajiwa katika maandamano hayo ya leo Ijumaa. Maandamano makubwa kwa baadhi, maandamano ya kuunga mkono utawala wa mpito kwa wengine, au hata kuunga mkono Maliba, ikimaanisha nchi kubwa ya Mali, waandaaji wanatarajia kuhamasisha watu wengi.

Ikiwa ratiba haitabadilika, kuanzia adhuhuri, watu watakusanyika katika katika eneo la Uhuru huko Bamako. Sala ya Ijumaa imepangwa kufanyika katika eneo hilo. Kisha, baada ya maandamano hayo, angalau viongozi saba wanatarajia kutoa hotuba zao, ikiwa ni pamoja na ile ya Waziri Mkuu Choguel Maïga. Inatarajiwa kwamba wadau wote watakosoa, kushutumu, vikwazo vya kisiasa na kiuchumi vilivyochukuliwa dhidi ya Mali katika mkutano wa mwisho wa Wakuu wa Nchi za ECOWAS.

Lakini maandamano hayo pia yanalenga kuonyesha umoja wa kitaifa ili kuondokana na mzozo huo. "Kinachotuunganisha ni bendera ya taifa," amesema mmoja wa waandalizi. Kwa upande wake, rais wa mpito, Kanali Assimi Goïta, hivi karibuni alithibitisha kwamba licha ya hali hiyo, nchi yake haina nia ya kukataa kushiriki mazungumzo na ECOWAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.