Pata taarifa kuu

Mvutano waendelea kati ya Algeria na Morocco

Algeria haijapinga habari iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari, ambayo inataja vyanzo vya kijeshi na kuripoti kupelekwa kwa vifaa vya kisasa vya kijeshi kwenye mpaka na Morocco, vilivyotengenezwa nchini Urusi.

Mpaka kati ya Morocco na Algeria (picha ya kilelezo).
Mpaka kati ya Morocco na Algeria (picha ya kilelezo). AFP PHOTO / FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Huu ni mfumo wa kwanza wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa ukubwa huu kutumwa barani Afrika. Inajumuisha kamera za kisasa zilizo na uwezo wa kuona usiku, zenye uwezo wa kutambua mienendo yote ya binadamu pamoja na rada. Mvutano ambao haujawahi kushuhudiwa kati ya nchi hizo mbili unazidi kuongezeka. Algiers na Rabat wanaonekana kushiriki katika mashindano ya silaha.

Mpaka kati ya Algeria na Morocco - uliofungwa kwa miaka 25 - ndio unaofuatiliwa kwa karibu zaidi kati ya nchi mbili za Kiarabu. Tangu kumalizika kwa uhusiano wao wa kidiplomasia msimu huu wa joto, Algeria inauchukulia mpaka wake na Morocco kama "sekta nyeti sana ya kijeshi". Hivi karibuni ilituma huko makombora.

Bora kudhibiti mpaka

Mamlaka ya Algeria inadai kutaka kudhibiti vyema mpaka huu. Kulingana na mamlaka hiyo, mifumo ya uangalizi iliyowekwa inanuiwa kupambana dhidi ya ulanguzi unaowanufaisha magaidi. Morocco inashutumiwa kwa kusafirisha mihadarati hadi nchini Algeria kupitia  mpaka wake ambapo jeshi la Morocco lilitumwa kwa mara ya kwanza siku chache zilizopita.

Mvutano umekuwa ukiongezeka tangu vifo vya madereva watatu kutoka Algeria wiki kadhaa zilizopita, waliouawa na ndege zisizo na rubani za Morocco karibu na Mauritania. Algiers ilikuwa imetishia kilipiza kisasi na ina wasiwasi hasa kuhusu kutiwa saini kwa mikataba kadhaa ya usalama kati ya Rabat na Tel Aviv kufuatia kurejeshwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Bajeti za kijeshi zinaongezeka

Algeria na Morocco zimeongeza bajeti zao za kijeshi kwa mwaka 2022 wakihofia makabiliano ya kijeshi. Kwa hivyo Rabat ilinunua mifumo ya ulinzi wa anga ya kisasa. Kuhusu Algeria, inajadiliana na Moscow - mshirika wake pekee - kupata makombora ya S500 na kizazi cha nne cha ndege ya Su-57 (jina la msimbo NATO Felon).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.