Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-USALAMA

Moto uliokuwa umezuka tena katika makao makuu makuu ya Bunge Cape Town wadhibitiwa

Bunge nchini Afrika Kusini limeteketea tena, saa 36 baada ya moto mkubwa kuharibu jengo hilo la kihistoria la miaka 130. Polisi tayari wamemkamata mshukiwa mwenye umri wa miaka 49 kuhusika na kitendo hiki na anatarajiwa kufikishwa Mahakama leo.

Moshi ukifuka kutoka makao makuu ya Bunge, ukumbi mkuu wa majengo ya Bunge la Afrika Kusini, baada ya moto uliozuka siku moja kabla ya kuanza tena Januari 3, 2022, huko Cape Town.
Moshi ukifuka kutoka makao makuu ya Bunge, ukumbi mkuu wa majengo ya Bunge la Afrika Kusini, baada ya moto uliozuka siku moja kabla ya kuanza tena Januari 3, 2022, huko Cape Town. RODGER BOSCH AFP
Matangazo ya kibiashara

Spika wa Bunge hilo, Nosiviwe Mapisa-Nqakula amesema kuteketea kwa Bunge sio jambo la kawaida.

Mamia ya maafisa wa idara ya zima moto walianza tena mapambano dhidi ya moto huo Jumatatu jioni, baada ya hali kua shwari wakati wa mchana.

Jumanne asubuhi, moto huo ulidhibitiwa tena baada ya kuanza tena Jumatatu jioni.

Mamlaka ilitangaza katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu kuwa moto huo ulidhibitiwa. Hata hivyo nusu saa baadaye, moshi mkubwa mweusi ulifuka tena kutoka kwenye paa na madirisha ya Bunge. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.