Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Moto mkali wateketeza jengo la Bunge mjini Cape Town

Jumapili hii, Januari 2, mjini Cape Town, moto umezuka katika jengo la mabunge mawili ya Bunge la Afrika Kusini, majengo yaliyoainishwa kama eneo la kihistoria na nchi hiyo.

Jengo la Bunge la Afrika Kusini ambapo moto ulizuka huko Cape Town, Januari 2, 2022.
Jengo la Bunge la Afrika Kusini ambapo moto ulizuka huko Cape Town, Januari 2, 2022. AFP - OBED ZILWA
Matangazo ya kibiashara
Moto huo ulizuka mwendo wa saa 11 Alfajiri kwa saa za Cpe Town katika eneo la mita chache kutoka Kanisa Kuu la St George ambapo mazishi ya Askofu Mkuu Desmond Tutu yalifanyika jana Jumamosi. Jengo la Bunge ambako wabunge wamekuwa wakiendesha vikao vyao limeharibiwa kabisa.

Moshi bado unafuka kutoka kwa vigae na madirisha juu ya paa ya hengo hili la Bunge. Maafisa wa Zima moto wanaendelea na shughuli ya yao kujaribu kudhibiti moto huo.

Jengo hili lilijengwa katika miaka ya 1885 na sasa maafisa wa idara ya Zima Moto wanajaribu kudhibiti moto ambao umeenea hadi makao makuu ya Baraza la Wawakilishi.

Majira ya saa sita mchana, Msemaji wa Bunge, Moloto Mothapo, amesema kuwa “ukumbi ambao wabunge walikuwa wanatumia kwa vikao” umeteketea kabisa kwa moto na kuongeza kuwa “moto bado haujazimika”.Moto huo haujasababisha maafa wala watu kujeruhiwa, mamlaka imesema. Rais Cyril Ramaphosa, ambaye amezuru eneo la tukio, amesema kusikitishwa na tukio hili mbaya, siku moja baada ya sherehe ya kumuaga Desmond Tutu.

Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto huu. Kwa mujibu wa mkuu huyo wa nchi, mtu mmoja alikamatwa na kusikilizwa na polisi.

Mji wa Cape Town umekumbwa na moto mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni. Mwezi Aprili, moto ulizuka katika Table Mountain, ukaenea hadi chuo kikuu kikuu cha jiji, na kuharibu maktaba yake ya thamani. Na mwezi mmoja kabla, moto ulizuka katika Bunge hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.