Pata taarifa kuu

Afrika Kusini yaanza rasmi maombolezo ya kitaifa hadi mazishi ya Desmond Tutu Januari 1

Baada ya taarifa za kifo cha Askofu Desmond Tutu, Afrika Kusini imetangaza rasmi maombolezo ya kitaifa, huku bendera zikiwa nusu mlingoti nchini kote na mbele ya balozi za Afrika Kusini kote duniani. Na hii hadi usiku wa mazishi ya mwanaharakati wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, yaliyopangwa kufanyika Januari 1, 2022, Rais Cyril Ramaphosa alitangaza Jumapili, Desemba 26.

Wapita njia wakiweka maua karibu na picha ya Askofu Mkuu Desmond Tutu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George mjini Cape Town? Desemba 26, 2021.
Wapita njia wakiweka maua karibu na picha ya Askofu Mkuu Desmond Tutu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George mjini Cape Town? Desemba 26, 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

"Kutakuwa na kipindi cha maombolezo wakati bendera ya taifa itakuwa nusu mlingoti," alisema wakati wa hotuba ya televisheni. "Hii itazingatiwa tangu kutangazwa kwa tangazo rasmi la mazishi yake na hadi jioni kabla ya" sherehe hizi, alisema.

Dakika chache baadaye, Wakfu wa Desmond Tutu ulitangaza kwamba mazishi ya Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana yatafanyika Jumamosi, Januari 1, 2022 huko Cape Town, katika Kanisa Kuu la St. George, parokia yake ya zamani. "Mipango ya wiki ya maombolezo bado haijapangwa vizuri," wakfu huo ulitangaza katika taarifa, huku ukibainisha "idadi ya matukio yaliyothibitishwa kwa wiki ijayo hadi mazishi ya" Askofu Mkuu "katika mji wa  Cape Town Jumamosi Januari 1, 2022. ".

Miongoni mwa vifungu vilivyotangazwa, wakfu huo unabaini kwamba "kengele za Kanisa Kuu la Mtakatifu George zitapigwa kila siku kwa dakika kumi, kuanzia saa sita mchana", wiki nzima kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Kifo cha Tutu kimekuja wiki chache tu baada ya kile cha rais wa mwisho wa enzi ya ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, FW de Klerk, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Siku ya Jumapili, Waafrika Kusini wa rika na asili mbalimbali walisimama karibu na Kanisa Kuu la St George's mjini Cape Town kuweka maua na kumuenzi shujaa huyo wa taifa hilo.

Tutu alitunukiwa tuzo ya Nobel mwaka 1984 kwa mchango wake katika mapambano ya kukomesha mfumo wa ubaguzi wa rangi uliotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia 1948-91.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.