Pata taarifa kuu

Mfahamu kiongozi wa kanisa aliyepinga ubaguzi wa rangi, Askofu Desmond Tutu

Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 90.  Askofu Desmond Tutu aliisaidia Afrika Kusini kumaliza ubaguzi wa rangi.

Maua karibu na picha ya Desmond Tutu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George huko Cape Town. Tarehe 26 Desemba 2021.
Maua karibu na picha ya Desmond Tutu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George huko Cape Town. Tarehe 26 Desemba 2021. AFP - GIANLUIGI GUERCIA
Matangazo ya kibiashara

Kifo cha Tutu kinajiri wiki chache tu baada ya Rais wa mwisho wa enzi za ubaguzi wa rangi FW de Clerk , kufariki akiwa na umri wa miaka 85.

Tutu alituzwa Tuzo ya Amani ya Nobel kufuatia mapambano yake yasiyo ya vurugu dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo mwaka 1984.

Askofu Tutu alishiriki katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi akishirikiana na Nelson Mandela, na kuchochea harakati za kukomesha sera ya ubaguzi wa rangi iliyotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia 1948 hadi 1991.

Alitawazwa kama padre mwaka wa 1960, na kuhudumu kama askofu wa Lesotho kuanzia 1976-78, askofu msaidizi wa Johannesburg na mkuu wa parokia ya Soweto.

Alikua Askofu wa Johannesburg mnamo 1985, na akateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza mweusi wa Cape Town.

Viongozi mbalimbali ulimwenguni wanaendelea kutuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini kilichotokea mapema leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.