Pata taarifa kuu

Askofu Desmond Tutu kuzikwa Januari Mosi

Mazishi ya Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Afrika Kusini, mwanaharakati wa muda mrefu dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo Desmond Tutu, yatafanyika Jumamosi Januari mosi huko Cape Town, katika Kanisa Kuu la St. George, parokia yake ya zamani, Wakfu wake ulitangaza Jumapili Desemba 26 jioni.

Askofu Mkuu Desmond Tutu katika uzinduzi wa kampeni ya haki za binadamu akati ikiadhimishwa miaka 60 tangu kusainiwa kwa Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, Desemba 10, 2007.
Askofu Mkuu Desmond Tutu katika uzinduzi wa kampeni ya haki za binadamu akati ikiadhimishwa miaka 60 tangu kusainiwa kwa Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, Desemba 10, 2007. REUTERS - Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Kifo cha Tutu kimekuja wiki chache tu baada ya kile cha rais wa mwisho wa enzi ya ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, FW de Klerk, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Afrika Kusini inafanya wiki ya matukio kuadhimisha kifo cha kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi Askofu Mkuu Desmond Tutu, aliyefariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 90.

Mipango hiyo ni pamoja na siku mbili za mwili wake kulala mahali maalum ili kutazamwa kabla ya mazishi rasmi ya serikali tarehe 1 Januari huko Cape Town.

Tutu alitunukiwa tuzo ya Nobel mwaka 1984 kwa mchango wake katika mapambano ya kukomesha mfumo wa ubaguzi wa rangi uliotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia 1948-91.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.