Pata taarifa kuu

Wiki ya sherehe za kumuenzi Desmond Tutu yaanza Afrika Kusini

Afrika Kusini inaingia wiki moja ya maombolezo kufuatia kutoweka kwa Desmond Tutu, aliyefariki dunia siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 90. Mwanaharakati huyo wa muda mrefu dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini atazikwa mnamo Januari Mosi katika mji wa kusini wa Cape Town.

Askofu Mkuu Desmond Tutu anaonekana kupitia umati wakati alipotembelea kituo cha vijana katika kitongoji cha Masiphelele, karibu na Cape Town, Afrika Kusini, Julai 8, 2011.
Askofu Mkuu Desmond Tutu anaonekana kupitia umati wakati alipotembelea kituo cha vijana katika kitongoji cha Masiphelele, karibu na Cape Town, Afrika Kusini, Julai 8, 2011. REUTERS - MIKE HUTCHINGS
Matangazo ya kibiashara

Wakfu wa Desmond Tutu ulitangaza kwamba mazishi ya Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana yatafanyika Jumamosi, Januari 1, 2022 huko Cape Town, katika Kanisa Kuu la St. George, parokia yake ya zamani.

Afrika Kusini imetangaza rasmi maombolezo ya kitaifa, huku bendera zikiwa nusu mlingoti nchini kote na mbele ya balozi za Afrika Kusini kote duniani. Na hii hadi usiku wa mazishi ya mwanaharakati wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, yaliyopangwa kufanyika Januari 1, 2022, Rais Cyril Ramaphosa alitangaza Jumapili, Desemba 26.

"Kutakuwa na kipindi cha maombolezo wakati bendera ya taifa itakuwa nusu mlingoti," alisema wakati wa hotuba ya televisheni. "Hii itazingatiwa tangu kutangazwa kwa tangazo rasmi la mazishi yake na hadi jioni kabla ya" sherehe hizi, alisema.

Wakfu wa Askofu Desmond Tutu ulibainisha katika taarifa kwamba  "idadi ya matukio yaliyothibitishwa kwa wiki ijayo hadi mazishi ya" Askofu Mkuu "katika mji wa  Cape Town Jumamosi Januari 1, 2022. ".

Miongoni mwa vifungu vilivyotangazwa, wakfu huo unabaini kwamba "kengele za Kanisa Kuu la Mtakatifu George zitapigwa kila siku kwa dakika kumi, kuanzia saa sita mchana", wiki nzima kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Tutu alitunukiwa tuzo ya Nobel mwaka 1984 kwa mchango wake katika mapambano ya kukomesha mfumo wa ubaguzi wa rangi uliotekelezwa na serikali ya wazungu wachache dhidi ya weusi walio wengi nchini Afrika Kusini kuanzia 1948-91.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.