Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Jeneza la Desmond Tutu lawasili katika Kanisa Kuu la Cape Town

Mwili wa Askofu Desmond Tutu umewasili Alhamisi asubuhi kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu George mjini Cape Town kwa ajili raia kutoa heshima za mwisho, kwa muda wa siku mbili, kwa mwanaharakati huyu aliyepambana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Katika Kanisa Kuu la Anglikana la St Mary's mjini Johannesburg, waumini wanatarajiwa kutoka heshima zao za mwisho kwa Desmond Tutu tarehe 29 na 30 Desemba 2021.
Katika Kanisa Kuu la Anglikana la St Mary's mjini Johannesburg, waumini wanatarajiwa kutoka heshima zao za mwisho kwa Desmond Tutu tarehe 29 na 30 Desemba 2021. AFP - LUCA SOLA
Matangazo ya kibiashara

Mazishi ya mwanaharakati huyo wa ubaguzi wa rangi yamepangwa kufanyika Jumamosi katika Kanisa Kuu la St George's mjini Cape Town, ambapo mwili wake umewasili leo Alhamisi asubuhi. Hapo awali, sherehe nyingi zilifanyika kote nchini. Huko Johannesburg, mishumaa iliwashwa Jumatano (Desemba 29) na manispaa ya jiji nje ya nyumba ya zamani ya Askofu huyu Mkuu huko Soweto. Misa iliandaliwa katika Kanisa lake kuu la zamani la St Mary's.

Ni katika kanisa hili pia ambapo Desmond Tutu alitawazwa kuwa Askofu wa Johannesburg mwaka wa 1985, mwaka mmoja kabla ya kuwa Askofu Mkuu. Sele anajivunia kuendelea kusali katika eneo hili linalohusishwa sana na historia ya mwanaharakati huu mkuu wa Afrika Kusini:

"Alifanya maisha yangu yabadilike. Nakumbuka vita vyake vya kupigania uhuru. Hauwa mfauasi au mjumbe wa chama chochote, alizingatia zaidi maandiko matakatifu. Hakika alikuwa mtu wa watu.

Askofu Desmond Tutu, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 90, Jumapili Desemba 26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.