Pata taarifa kuu

Algeria: Sonatrach kuwekeza dola bilioni 40 kwa miaka mitano

Nchini Algeria, kampuni kubwa ya mafuta, Sonatrach, itawekeza kiasi sawa cha dola bilioni 40 katika miaka mitano ijayo ili kuendeleza uzalishaji na usafishaji wa hidrokaboni.

Nembo ya kampuni inayomilikiwa na serikali ya Algeria ya Sonatrach, Algiers, Novemba 25, 2019.
Nembo ya kampuni inayomilikiwa na serikali ya Algeria ya Sonatrach, Algiers, Novemba 25, 2019. © Ramzi Boudina/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mwaka wa 2021,kampuni hiyo, ambayo ilikuwa imepunguza uwekezaji wake kufuatia mgogoro wa Covid-19, inakusudia kusonga mbele. Sonatrach ni nguzo ya uchumi wa Algeria. Kampuni hii huchangia 40% katika hazina ya serikali.

Kwa peke yake, Toufik Hakkar ana uwezo wa kurejesha hali halisi ya uchumi wa Algeria. Akitanga kwenye kituo cha televisheni cha AL24 mpango kabambe wa uwekezaji, Mkurugenzi Mkuui wa kampuni ya Sonatrach amenyamazisha uvumi kuhusu kuzorota kwa shughuli ya kampuni kubwa ya hidrokaboni ya Algeria.

Kwa miaka ishirini uzalishaji umepungua, hasa katika sekta ya mafuta, kwa ukosefu wa uwekezaji wa kutosha. Na upunguzaji wa bajeti ulioagizwa mwaka wa 2020 na rais Tebboune ulitia wasiwasi jumuiya ya wafanyabiashara.

Lakini mwaka wa 2021 Sonatrach iliona mapato yake ya mauzo ya nje yakiongezeka 74% hadi kufikia dola 34.5 bilioni. Imebadilisha wasambazaji wake, haswa kwa kupata zaidi kutoka kwa soko la ndani. Pia imerekebisha gharama zake, na sasa inapanga kuzindua upya utafutaji wa madini na usafishaji.

Kiwanda cha kusafishia mafuta kitajengwa Hassi Messaoud na kile cha Skikda lazima kipanuliwe. Sonatrach, ambayo imepata faida za kodi kwa wawekezaji, inakusudia kuvutia washirika zaidi. Theluthi moja ya uwekezaji wa bilioni 40 uliopangwa utahusu makampuni ya kigeni ya mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.