Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Somalia: UNSC yaongeza muhula wa AMISOM wa miezi mitatu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hatimaye limeongeza muda wa majukumu ya AMISOM, Ujumbe wa Umoja wa Afrika Kupambana na wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabab nchini Somalia, kwa kipindi cha miezi mitatu. Hali hiyo ilikuwa inatarajiwa.

Wanajeshi wa AMISOM waliotumwa Somalia.
Wanajeshi wa AMISOM waliotumwa Somalia. Reuters/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Marekebisho ya ujumbe huu, ambayo kila mtu anataka yafanyike, yanacheleweshwa na tofauti kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa hasa juu ya mustakabali wa ujumbe huu.

Kwa miezi kadhaa, majadiliano yamekuwa yakifanyika kati ya Somalia, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuhusu mageuzi ya kimsingi ya AMISOM ambayo wote wanaona ni muhimu, lakini ambayo hawawezi kukubaliana nayo. Kuongeza muda wa mamlaka ya sasa kwa miezi mitatu kwa hiyo ni njia ya kujipa muda wa kutumaini kufikia mwafaka.

Tofauti za ukubwa

Je, wakati huu utatosha? Hakuna Uhakika wowote, kwa sababu tofauti ni kubwa. Somalia inataka kujiondoa haraka kutoka kwa ujumbe huo ifikapo mwaka 2023 na kupewa mamlaka zaidi kwa jeshi la taifa katika vita dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.

Umoja wa Afrika, kwa upande wake, unataka ujumbe wa mseto uwe chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa. Hii itairuhusu kuwa tegemezi kidogo kifedha kwa Umoja wa Ulaya, mfadhili mkuu wa ujumbe huo ambayo inaonyesha dalili za kutoshirikishwa, lakini chaguo hili pendekezo imefutiliwa mbali na Umoja wa Mataifa.

Mgogoro wa kina

Ushahidi kwamba mgogoro ni mkubwa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa walipaswa mwezi Septemba kutoa ripoti ya pamoja juu ya mustakabali wa ujumbe huo, lakini hatimaye kila mmoja aliandika ripoti yake. Jumanne wiki hii, baada ya upigaji kura, Marekani na Ufaransa hasa hazikuficha kusema kuwa faili hili lilicheleweshwa na kusisitiza kwamba muda wa miezi mitatu utakuwa wa mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.