Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Somalia: Mlipuko waua angalau watano, na kujeruhi ishirini na tatu Mogadishu

Takriban watu watano wamefariki na wengine 23 kujeruhiwa baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,mapema Alhamisi, kulingana na maafisa na shahidi mmoja kwa mujibu wa tovuti ya shirika la utangazaji la VOA .

Mabasi ya shule yaliyoharibika yanaonekana katika eneo la tukio baada ya gari kulipuka katika shambulio la kujitoa mhanga karibu na shule ya msingi na sekondari ya Mucassar katika wilaya ya Hodan ya Mogadishu, Somalia Novemba 25, 2021.
Mabasi ya shule yaliyoharibika yanaonekana katika eneo la tukio baada ya gari kulipuka katika shambulio la kujitoa mhanga karibu na shule ya msingi na sekondari ya Mucassar katika wilaya ya Hodan ya Mogadishu, Somalia Novemba 25, 2021. © REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

"Hadi sasa, tunajua kwamba watu watano wamefariki na wengine 23 (wamejeruhiwa)," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa huduma za gari za wagonjwa huko Aamin, ameliambia shirika la habari la REUTERS.

Kundi la Kiislamu la Somalia la Al Shabab, wahusika wa shambulio hilo, lilikuwa likilenga msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa uliokuwa ukipita, amesema Abdiasis Abu Musab, msemaji wa operesheni za kijeshi za kundi hilo.

Mlipuko huo, ambao ulitokea karibu na makutano ya barabara K4 katikati ya Mogadishu, ulikuwa mkubwa sana hadi uliangusha kuta za shule ya msingi na sekondari ya Mucassar iliyo karibu.

"Tulitikiswa na ukumbwa wa mlipuko, kisha kukasikika milio ya risasi," amesema Mohamed Hussein, muuguzi katika hospitali jirani ya Osman.

Ameongeza kuwa alitolewa kwenye vifusi vya dari iliyoporomoka.

“Kuta za hospitali yetu zimeanguka, mbele yetu kuna shule ambayo nayo imeanguka sijui ni watu wangapi waliofariki,” amesema.

Maafisa wa usalama hawakupatikana mara moja ili kutoa maoni yao.

Al Shabab wanapigana kwa miaka mingi dhidi ya serikali kuu ya Somalia kuanzisha utawala wake kwa kuzingatia tafsiri yake kali ya sheria za kiislamu za Sharia.

Kundi hilo mara kwa mara hufanya mashambulizi ya mabomu na mashambulizi kwa kutumia silaha nchini Somalia na kwingineko katika vita vyake dhidi ya jeshi la Somalia na kikosi cha Umoja wa mataifa cha AMISOM, ambacho kinasaidia kuilinda serikali kuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.