Pata taarifa kuu
TUNISiA-UCHAGUZI

Rais Saïed aongeza muda wa kusitishwa kwa Bunge na kutangaza kura ya maoni

Wakati nchi ya Tunisia inapojiandaa kusherehekea miaka kumi na moja ya mapinduzi yake wiki hii, Rais Kaïs Saïed, ambaye alichukua mamlaka kamili mwezi Julai imwaka huu, alihutubia taifa jioni ya Jumatatu, Desemba 13. Alikataa mfululizo wa hatua zinazoimarisha zaidi mamlaka yake.

Rais wa Tunisia Kaïs Saïed,  Desemba 8, 2021.
Rais wa Tunisia Kaïs Saïed, Desemba 8, 2021. AP - Slim Abid
Matangazo ya kibiashara

Kama kawaida, Kaïs Saïed aliwashangaza wengi. Wakati hotuba yake ilitarajiwa Desemba 17 - tarehe ya kuadhimishwa kwa tukio la Mohamed Bouazizi la kujichoma kwa moto, hali ambayo iliashiria kuanza kwa mapinduzi ya mwaka 2011 - rais wa Tunisia, inaonekana, amependelea kuharakisha hali ya mambo nchini mwake.

Miezi minne na nusu baada ya kuchukua mamlaka kamili, Rais Kaïs Saïed hatimaye alielezea ajenda yake.

Uchaguzi wa wabunge kufanyika tarehe 17 Desemba 2022

Makataa ya kisiasa yatafayika mwaka 2022, mchakato ambao utaanza na mashauriano ya kiraia na ya kielektroniki kuanzia mwezi Januari hadi Machi. Kura ya maoni kuhusu rasimu ya Katiba iliyorekebishwa itafanyika tarehe 25 Julai. Kisha, uchaguzi wa wabunge utafanyika kuanzia tarehe 17 Desemba 2022.

Wakati huo huo, Bunge la Tunisia bado limezuiwa kufanya shughuli yoyote. Wapinzani wa Rais Saïed tayari wamepanga kupinga hatua hizi kwa kuitisha maandamano Ijumaa ijayo Desemba 17, tarehe ya maadimisho ya mwaka wa kumi na moja wa mapinduzi ya Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.