Tunisia: Rais aahidi kuteua serikali na kufanyia marekebisho Katiba
Baada ya hali ya hatari kutangazwa Julai 25, rais wa Tunisia Kaïs Saïed, hatimae, anataka kufanyia marekebisho Katiba ya 2014. Hivi ndivyo alisema, Jumamosi jioni Septemba 11, akitangaza, wakati huo huo, kuundwa kwa serikali hivi karibuni.
Imechapishwa:
Akiongea na wafuasi wake na vyombo vichache vya habari, Kaïs Saïed aliweka wazi nia yake. Alizungumzia kuhusu marekebisho ya Katiba.
“Lazima tufanye mabadiliko katika mfumo wa Katiba. Katiba sio za milele, zinaweza kubadilishwa! Mabadiliko yanapaswa kuwafaa raia wa Tunisia, kwa sababu baada ya yote, mamlaka ni yao, ”alisema. Na ili marekebisho yake ya katiba yapitishwe, Kaïs Saïed kwa hivyo alisema atatumia kura ya maoni.
Mkuu wa Nchi pia yuko mbioni kutangaza serikali mpya: "Ninawahakikishia kwamba watu watakaoteuliwa watakuwa waaminifu, ambao hawatokwenda kinyume na ahadi zao," alisema. Wiki saba zilizopita, Bwana Saïed alichukua madaraka yote ya kiutendaji na kusitisha shughuli za bunge.