Pata taarifa kuu
TUNISiA-SIASA

Tunisia: Rais Kais Saied aongeza muda wa kusitishwa kwa shughuli za bunge

Rais wa Tunisia Kais Saied amesema shughuli za bunge zitaendelea kusitihwa "hadi itakapo chukuliwa hatua nyingine". Shughuli za bunge la Tunisia zimesitishwa shwa tangu mapinduzi ya Julai 25, ambayo yalimuwezesha Bwana Saied kuchukua mamlaka yote.

Kaïs Saïed, rais wa Tunisia.
Kaïs Saïed, rais wa Tunisia. Anis Mili/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Julai 25, Saied alidai kuwa hatua aliyochukuwa inakwenda sambamba na katiba ya nchi kwa kujipa mamlaka kamili, kwa kumfukuza kiongozi wa serikali, Hichem Mechichi, na kusimamisha shughuli za bunge kwa kipindi cha siku 30.

Hata kabla ya kumalizika kwa kipindi hiki, Bwana Saied "ametoa agizo lingine la kirais kongeza muda wa hatua hii kuhusiana na kuitishwa kwa shughuli za bunge na vile vile kuondoa kinga ya wabunge wote hadi itakapochukuliwa hatua nyingine", ofisi ya rais imebaini katika taarifa fupi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Uamuzi huu haukuwashangaza wengi. Mbali na kuongezwa kwa muda wa kusitishwa shughuli za bunge, wachambuzi walikuwa wanasubiri rais Saied kutangaza hatua mpya ili kutuliza nyoyo raia na pia kuhakikishia jamii ya kimataifa.

Tangu mapinduzi yake, Rais Saied bado hajateua serikali mpya au kuzindua "muongozo" unaodaiwa na vyama kadhaa vya kisiasa na mashirika ya kiraia.

"Rais atalihutubia taifa katika siku zijazo," ofisi ya rais imeongeza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, bila maelezo zaidi.

Mnamo Julai 25, Bwana Saied alitangaza kwamba anachukua mamlaka ya kiutendaji serikalini, kwa "msaada wa serikali" ambayo itaongozwa na waziri mkuu mpya atayeteua.

Uamuzi wake umelaaniwa kama "mapinduzi" na baadhi ya wanasheria na vile vile na wapinzani wake, hasa chama cha Kiislamu cha Ennahdha, chenye viti vingi bungeni katika nchi hiyo ambayo imeendelea kukumbwa na changamoto za kisiasa kwa miezi kadhaa.

Bwana Saied amekuwa akijitetea mara kwa mara kwamba alichukuwa hatua hiyo kulingana na "sheria" na Katiba iliyopitishwa mnamo mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.