Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA

Tunisia: Wabunge watatu wanaomkosoa rais Kaïs Saïed wakamatwa

Tunisia inaendelea kusubiri uteuzi wa wazirimkuu baada ya rais wa nchi hiyo kuchukuwa hatu ya kuvunja serikali na kusitisha shughuli za Bunge.

Kikao cha Bunge la Tunisia Desemba 2, 2014, huko Tunis.
Kikao cha Bunge la Tunisia Desemba 2, 2014, huko Tunis. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Rais Kaïs Saïed ameendelea kuchukuwa hatua katika hali ya kujidhatiti mamlakani. Kuondolewa kinga kwa wabunge kadhaa na kuvunjwa kwa Bunge nii miongoni mwa hatua zilizochukuliwa hivi punde. Na wiki hii wabunge kadhaa walikamatwa.

Wabunge wawili wwa chama cha Kiislamu cha Al Karama, mshirika wa chama cha Ennahdha, walikamatwa, kiongozi wa chama hicho alitangaza Jumapili Agosti 1. Maher Zid na Mohamed Affes wako kizuizini kwa ajili ya "uchunguzi wa mahakama ya kijeshi", kiongozi wa chama cha Al Karama ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Mapema wiki, mbunge huru Yassine Ayari pia alikamatwa.

Wote wana msimamo mmoja wa kukosoa na kulaani hatua zilizochukuliwa Jumapili iliyopita na Rais Saïed, ambao wanaamini kuwa ni "mapinduzi".

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu Human Right Watch wiki hii lilielezea hofu yake kwamba "kuna hatari rais Saïed atumie mamlaka yake dhidi ya wapinzani wake." Kaïs Saïed alisema Ijumaa kuwa watu wasiwe na "hofu" kuhusu uhuru na haki nchini Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.