Pata taarifa kuu
TUNISiA-SIASA

Mgogoro wa kisiasa Tunisia: chama cha Ennahdha chataka uchaguzi wa mapema

Baada ya kufutwa kazi na rais Jumapili, Hichem Mechichi, ambaye alikuwa waziri mkuu wa Tunisia, amesema yuko tayari kuachilia madaraka.

Kiongozi wa chama cha Ennahdha, Rached Ghannouchi, huko Tunis, Februari 2021.
Kiongozi wa chama cha Ennahdha, Rached Ghannouchi, huko Tunis, Februari 2021. REUTERS - ZOUBEIR SOUISSI
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa chama kikuu bungeni, Ennahdha, ambacho kinamuunga mkono, kimelaani kile kilichoita mapinduzi, lakini baada ya kikao cha kamati kuu ya chama kilichofanyika usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, chama hicho kimeomba uchaguzi wa mapema.

Chama cha Ennahdha, chama kikuu chenye viti vingi Bungeni, kinasema kiko tayari "kwa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema wa wabunge na urais kuhakikisha usalama wa mchakato wa kidemokrasia, ili kuzuia ucheleweshaji wowote kutumiwa kama kisingizio cha kudumisha utawala wa kiimla.

Chama cha Kiislam hata hivyo kinaendelea kulaani "mapinduzi dhidi ya Katiba na taasisi. Kiongozi wa chama hicho, Rached Ghannouchi, alipiga kambi kwa masaa kumi na mbili Jumatatu mbele ya Bunge, akizungukwa na jeshi, kudai aweze kuingia bungeni.

Kwa upande wake, kwa hotuba yake ya kwanza tangu kutangazwa kufutwa kazi, Waziri Mkuu Hichem Mechichi amekubali uamuzi wa Mkuu wa Nchi, Kaïs Saïed kumfuta kazi. "Niko tayari kukabidhiwa madaraka kwa mtu ambaye atateuliwa na rais wa Jamhuri", amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.