Pata taarifa kuu
TUNISiA-SIASA

Makabiliano yazuka Tunisia baada ya Rais Saïed kuvunja serikali

Siku moja baada ya uamuzi wa rais Kaïs Saïed kuvunja serikali na kusitisha shughuli za Bunge na kumfukuza kazi Waziri Mkuu Hichem Mechichi, wafuasi wa kiongozi wa chama cha Ennahdha, kinachoongoza Bunge, walikusanyika Jumatatu mbele ya Ikulu ya Bardo huko Tunis. Wamekabiliana na wafuasi wa rais Saïed, hali ambayo ilisababisha makabiliano.

Mvutano wainuka katika jiji la Tunis, Tunisia, Julai 26, 2021
Mvutano wainuka katika jiji la Tunis, Tunisia, Julai 26, 2021 AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi, wakati kambi mbili zilikutana na kukabiliana mbele ya makao makuu ya Bunge Jumatatu asubuhi.

Upande mmoja polisi imeweka vizuizi, huku wafuasi wa Kaïs Saïed wakidai maamuzi yaliyochukuliwa Jumapili na rais ni halali. Kwa upande mwingine, wafuasi wa chama cha Ennahdha na kiongozi wake Rached Ghanouchi ambao, kwa upande wao, wakibaini kwamba maamuzi hayo ni shambulio dhidi ya demokrasia na pia ni jaribio la mapinduzi.

Saïed amechukua hatua hiyo kufuatia miezi kadhaa ya mivutano kati yake na Waziri Mkuu Hichem Mechichi, pamoja na Bunge lililogawanyika. Hayo yanajiri katika wakati ambapo Tunisia inakabiliana na mgogoro wa kiuchumi uliozidishwa na janga la COVID-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.