Pata taarifa kuu
TUNISiA-SIASA

Tunisia: Maandamano yalenga chama cha Ennahda

Polisi na waandamanaji wamekabiliana katika miji kadhaa ya Tunisia siku ya Jumapili wakati wapinzani wakitaka serikali ijiuzulu, huku wakishambulia ofisi za chama cha Kiislam chenye msimamo wa wastani, Ennahda, chama kikubwa zaidi cha kisiasa chenye wahumbe wengi bungeni.

Makabiliano yalizuka wakati mamia ya waandamanaji walikusanyika katika kila moja ya miji mikubwa ya Tunisia, katikati ya visa vingi maambukizi ya COVID-19 ambavyo vinazidisha mgogoro wa kiuchumi wa nchi hiyo na kuonyesha jinsi gani siasa kwa vyama vya siasa imekuwa ngumu.
Makabiliano yalizuka wakati mamia ya waandamanaji walikusanyika katika kila moja ya miji mikubwa ya Tunisia, katikati ya visa vingi maambukizi ya COVID-19 ambavyo vinazidisha mgogoro wa kiuchumi wa nchi hiyo na kuonyesha jinsi gani siasa kwa vyama vya siasa imekuwa ngumu. FETHI BELAID AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashahidi, waandamanaji walijaribu kuvamia au hata kushikilia ofisi za chama cha Ennahda huko Monastir, Sfax, El Kef na Sousse, wakati huko Touzeur walichoma moto makao makuu ya chama.

Makabiliano yalizuka wakati mamia ya waandamanaji walikusanyika katika kila moja ya miji mikubwa ya Tunisia, katikati ya visa vingi maambukizi ya COVID-19 ambavyo vinazidisha mgogoro wa kiuchumi wa nchi hiyo na kuonyesha jinsi gani siasa kwa vyama vya siasa imekuwa ngumu.

Maandamano hayo, ambayo ni makubwa zaidi nchini Tunisia tangu miezi kadhaa iliyopita, yalisababishwa na wanaharakati kwenye mitandao ya kijamii. Hakuna chama cha siasa kilichowaunga mkono hadharani.

Huko Tunis, polisi walitumia gesi ya pilipili dhidi ya waandamanaji ambao walikuwa wakirusha mawe na kupiga makelele wakidai kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Hichem Mechichi na kuvunjwa kwa Bunge. Maandamano mengine makubwa yalifanyika huko Gafsa, Sidi Bouzid na Nabeul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.