Pata taarifa kuu

Polisi wakabiliana na waandamanaji vijana katika mji mkuu Tunisia

Mapigano makali yalizuka Jumamosi kati ya vikosi vya usalama vya Tunisia na mamia ya waandamanaji wengi wao wakiwa ni vijana ambao waliingia kwenye barabara za katikati mwa mji mkuu Tunis kuonyesha hasira yao dhidi ya idadi kubwa ya ukatili unaotekelezwa na polisi katika vitongoji vya wafanyikazi wa Tunisia

waandamanaji katika mtaa wa Sidi Hassine, kitongoji cha Tunis, le Jumamosi Juni 12 usiku
waandamanaji katika mtaa wa Sidi Hassine, kitongoji cha Tunis, le Jumamosi Juni 12 usiku AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Picha kutoka katika mji mkuu,zinaonyesha waandamanaji walionekana wakirusha miti, viti na chupa za maji kwa vikosi vya usalama ambao nao walifyatua gesi za kutoa machozi na kuwazuilia takriban watu kadhaa.

Maandamano hayo ya Jumamosi yamekuja ikiwa ni siku tatu mfululizo wa mvutano ulianza baada ya kijana mmoja kuuawa "katika mazingira tatanishi" katika eneo la Sidi Hassine Sijoumi nje kidogo ya jiji la Tunis, kulingana na shirika linalotetea Haki za Binadamu nchini Tunisia (LTDH).

Machafuko hayo pia yalisababishwa na shambulio lililotokea siku ya Alhamisi, ambapo mtoto mdogo alivuliwa uchi na kupigwa vibaya na vikosi vya polisi katika eneo hilo. tukio hilo lilisambaa kupitia video kwenye mitandao ya kijamii. Tukio hilo lilizua ghadhabu kubwa  kwa wananchi na baada ya hapo awali polisi kutoa taarifa kwamba kijana huyo aliyepigwa kwenye video alikuwa amelewa,

Wizara ya Mambo ya Ndani imekiri maafisa wake kuhusika na shambulio hilo na kuhakikisha wamesimamishwa kazi. Katika taarifa yake, LTDH ililaani vurugu zilizowapata raia wakati wa mapigano na polisi "ili kuzima sauti za maandamano", kwa kumlaumu Waziri Mkuu Hichem Mechichi - ambaye pia ni waziri wa mpito wa mambo ya ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.