Pata taarifa kuu
TUNISiA

Wahamiaji 57 wafariki dunia katika ajali ya meli kutoka Tunisia

Takriban waomba hifadhi 57 kutoka Libya wamefariki dunia baada ya boti waliokuemo kuzama kwenye pwani ya Tunisia walikuwa wanapojaribu kuingia nchini Italia, shirika la hilali nyekundu limesema leo Jumanne.

Wahamiaji wanapumzika baada ya kushuka kwa meli katika kisiwa cha Mediterranean cha Lampedusa, Italia Mei 11, 2021.
Wahamiaji wanapumzika baada ya kushuka kwa meli katika kisiwa cha Mediterranean cha Lampedusa, Italia Mei 11, 2021. REUTERS - ANTONIO PARRINELLO
Matangazo ya kibiashara

"Watu thelathini na tatu wameokolewa," Mongi Slim, afisa wa shirika hilo la kibinadamu, ameliambia shirika lahabari la REUTERS.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez ameamua kusitisha safari yake iliyopangwa kwenda Paris Jumanne hii  (Mei 18) kwa sababu ya mgogoro uliosababishwa na maelfu ya wahamiaji katika eneo la Ceuta la Uhispania, serikali yake imesema katika taarifa.

Kwa sababu ya "matukio ya hivi karibuni" huko Ceuta, Bwana Sanchez amekata kuhudhuriia katika mkutano juu ya ufadhili wa uchumi wa Afrika katika mji mkuu wa Ufaransa na atazungumza mwishoni mwa kikao cha baraza la mawaziri saa sita mchana, serikali ya Uhispania, ikinukuliwa na shirika la habari la AFP, imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.