Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA

Maaumuzi ya rais Kais Saied yaendelea kuzua sintofahamu nchini Tunisia

Rais wa Tunisia Kais Saied ameendelea kuwaachisha kazi maafisa wa juu serikali, siku chache baada ya kumfuta kazi waziri mkuu na kusitisha shughuli za bunge, hatua ambayo inaendelea kuzua sintofahamu ya kisiasa nchini humo.

Rais wa Tunisia Kaïs Saïed amehutubia taifa, lakini ameshindwa kujibu maswali yote.
Rais wa Tunisia Kaïs Saïed amehutubia taifa, lakini ameshindwa kujibu maswali yote. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kumfuta kazi waziri mkuu na waziri wa ulinzi na masuala ya sheria, rais Said sasa amemfuta kazi Mkurugenzi Mkuu wa Televisheni ya taifa Wataniya.

Akizungumza siku ya Jumatano, kiongozj huyo wa Tunisia pia amemfuta kazi mkuu wa mashtaka ndani ya jeshi la nchi hiyo, wakati huu akiondoa kinga dhidi ya wabunge na kujipatia madaraka ya Mahakama.

Hatua hii inakuja wakati huu mashirika ya kiraia na wapinzani wa kiongozi huyo wakiendelea kusema kinachoendelea ni kama mapinduzi ya kijeshi.

Chama cha Kiislamu chenye mrengo wa Kati Ennahdha, tayari kimesema, kipo tayari kwa uchaguzi mpya, wa wabunge na rais, iwapo sintofahau hiyo itaendelea.

Rais Said mwenye umri wa miaka 63, ametetea uamuzi wake anaosema, amepewa nguvu na katiba ya nchi hiyo kuchukua hatua hiyo iwapo serikali ipo kwenye hatari, wakati huu anapoendelea kupata shinikizo kutoka mataifa ya nje, kama Ufaransa, kuteua serikali mpya haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.