Pata taarifa kuu
TUNISiA-SIASA

Tunisia: Rais wa zamani Marzouki adai kushtushwa na waranti wa kukamatwa dhidi yake

Jaji wa Tunisia alitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa Alhamisi, Novemba 4 dhidi ya rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki, mkosoaji mkubwa wa mapinduzi ya mkuu wa sasa wa nchi Kaïs Saïed. Kwa sasa Moncef Marzouki anaishi Ufaransa.

Jaji wa Tunisia alitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa Alhamisi, Novemba 4 dhidi ya Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki, anayeishi Ufaransa na ambaye anakosoa vikali mapinduzi ya mkuu wa sasa wa nchi Kaïs Saïed.
Jaji wa Tunisia alitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa Alhamisi, Novemba 4 dhidi ya Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki, anayeishi Ufaransa na ambaye anakosoa vikali mapinduzi ya mkuu wa sasa wa nchi Kaïs Saïed. - Ettounsiya TV channel/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa jaji huyo unakuja baada ya rais Saïed kuzitaka mahakama za Tunisia katikati ya mwezi wa Oktoba kufungua uchunguzi kuhusu kauli za Bw. Marzouki na kuzuia hati yake ya kidiplomasia ya kusafiria. Moncef Marzouki ambaye anachukulia kama "msaliti kwa nchi" na rais Saïed, anasema ameshangazwa na uamuzi huu wa vyombo vya sheria vya Tunisia.

"Hii inanishtua sana, kwa sababu inaongeza mzozo nchini na ninaamini kuwa agizo hili la kimataifa, ambalo ni la kushangaza kabisa, tu, kwa usahihi, linaimarisha taswira ya udikteta, zaidi ya udikteta wa kila mahali," Moncef Marzouki amesemaakihojiwa na Houda Ibrahim, wa kitengo cha RFI kanda ya Afrika (RFI Afrique).

Kwa mujibu wa rais wa zamani, Tunisia inastahili mambo mazuri zaidi kuliko hayo.

Mheshimiwa huyu alipochaguliwa kwa miaka miwili sikufungua kinywa changu, kwani najua jinsi inavyokuwa vigumu kwa rais kutumia madaraka. Sikutaka kamwe kuchochea uhasama. Lakini wakati kulikuwa na mapinduzi, kwangu haikukubalika. Kila kitu nilichopigania maisha yangu yote, yaani utawala wa sheria, demokrasia, uhuru n.k., kimetupwa kwenye takataka. Kwa hivyo nilichukua msimamo mara moja, nikisema kwamba kukubali mapinduzi haya ni jambo lisilofaa. Na kisha, mtu huyu alipoingia ndani zaidi katika mapinduzi haya, niliishia kusema: Mtu huyu, tunapaswa kumzuia, tunapaswa kumuweka chini na lazima ahukumiwe. 
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.