Tunisia: Maandamano dhidi ya rais Kaïs Saïed yafanyika chini ya uangalizi mkubwa
Maandamano mapya yamefanyika huko Tunis, Jumapili hii, Oktoba 10. Maelfu ya wfuasi wa uapinzani wa rais wa Tunisia Kaïs Saïed walimiminika mitaani wakidai rais huyo ajiuzulu.
Imechapishwa:
Hata kabla ya kuwasili kwenye mtaa wa Bourguiba, eneo la maandamano dhidi ya Rais Saïed, maelfu ya maafisa wa polisi walikuwa wamezingira eneo hilo. Maandamano ya wapinzani wa rais yamefanyika chini ya uangalizi mkubwa.
Mamlaka ilikuwa imepiga marufuku ya maandamano kufanyika katika baadhi ya mitaa, pia marufuku kwa waandishi wa habari kukaribia maandamano hayo. Maafisa wa polisi waliokuwa wamepiga kambi karibu na eneo la maandalano waliwataka waandamanaji kurudi nyuma.