Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA

Tunisia: Najla Bouden apewa jukumu la kuunda serikali mpya

Rais wa Tunisia Kais Saied amempa jukumu la kwanza mwanamke, Najla Bouden, kuunda serikali nchini Tunisia, miezi miwili baada ya baraza la mawaziri la awali kutimuliwa, ofisi ya rais wa Tunisia imetangaza Jumatano hii Septemba 29.

Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden Romdhane.
Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden Romdhane. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Bi Bouden "amepewa jukumu la kuunda serikali haraka iwezekanavyo," imesema taarifa kutoka ofisi ya rais.

Bi Bouden ambaye alizawa mwaka wa 1958 na mwanasayansi aliyebobea, ambaye ana umri sawa na rais Kais Saied ni kutoka mji wa Kairouan, na si maarufu sana nchini humo.

Ni mara ya kwanza kwa mwanamke kuchukua wadhifa huu wa kiongozi wa serikali nchini Tunisia, hata kama jukumu alilopewa limepunguzwa nguvu sna "hatua za kipekee" zilizoidhinishwa na Bwana Saied Septemba 22, ambazo zinasitisha utekelezaji wa ibara kuu za Katiba.

Ofisi ya rais imetoa video ya Bwana Saied akimpokea Bi Bouden ofisini kwake na kumuelekeza aunde serikali mpya na kuweza kuiwasilisha kwake "katika masaa au siku chache zijazo".

Bwana Saied amesisitiza mara kadhaa juu ya asili "ya kihistoria" ya uteuzi wa mwanamke kwa mara ya kwanza kuongoza serikali nchini Tunisia. "Ni heshima kwa Tunisia na ni heshima kwa wanawake wa Tunisia."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.