Pata taarifa kuu
DRC-UFISADI

Congo Hold-up: Mjasiriamali kutoka Ubelgiji ahusishwa katika ufisadi mkubwa DRC

Mfanyabiashara Philippe de Moerloose, aliyeteuliwa kuwania tuzo ya meneja bora wa mwaka nchini Ubelgiji, hajajitajirisha tu kwa kuuza vifaa vya mamlaka ya Congo kwa viwango vya faida zaidi ya wastani? bali pia aliweza kuchukua fursa ya kutoza ushuru maradufu.

Mfanyabiashara wa Ubelgiji Philippe de Moerloose anatajwa katika uchunguzi wa Congo Hold-up.
Mfanyabiashara wa Ubelgiji Philippe de Moerloose anatajwa katika uchunguzi wa Congo Hold-up. © RFI/Le Soir/De Standaard
Matangazo ya kibiashara

Katikati ya wilaya tajiri zaidi ya Kinshasa, Gombe, hoteli ya Pullman inamilikiwa nusu na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo mara nyingi hutumiwa kwa makongamano.

Asilimia 50 iliyosalia iliuzwa mwaka wa 2010 kwa mfanyabiashara wa Ubelgiji, Philippe de Moerloose, kupitia kampuni iliyoanzishwa katika mojawapo ya maeneo yenye kutoza ushuru zaidi duniani: Visiwa vya Virgin vya Uingereza.

Philippe De Moerloose ni mmoja wa watu 150 tajiri zaidi nchini Ubelgiji. Kundi lake, ambalo linajishughulisha na usambazaji wa vifaa vizito kama vile malori, matrekta, mashine za kuchimba madini, linatarajia kupata mauzo ya euro bilioni moja mwaka huu.

Aliteuliwa mnamo mwezi Novemba kwa mara ya pili mfululizo kwa tuzo ya "meneja wa mwaka" kutoka kwa jarida la biashara la Ubelgiji, Trends.

Lakini safari yake ya mafanikio ilijengwa kutokana na kandarasi kubwa zilizotiwa saini na mamlaka ya DRC chini ya utawala wa rais wa zamani Joseph Kabila, ambaye aliondoka madarakani Januari 2019.

Uchunguzi wa Congo Hold-up, kulingana na uvujaji wa hati za siri za benki milioni 3.5 zilizofichuliwa kwamba alikuwa ametengeneza mamia ya mamilioni ya dola katika koloni hili la zamani la Ubelgiji kwa kuweka ushuru wa kizuwizi kwa ununuzi wa mitambo yake ya ujenzi na matrekta – madai ambayo amekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.