Pata taarifa kuu

Afrika Kusini yatoa heshima za mwisho rasmi kwa rais wa zamani Frederik de Klerk

Nchini Afrika Kusini, Rais Cyril Ramaphosa ameongoza raia wa nchi hiyo katika mazishi ya kitaifa, kumwaga Frederik Willem De Klerk, aliyekuwa rais wa mwisho wa serikali iliyoendeleza mfumo wa ubaguzi wa rangi, kati ya mwaka 1989 hadi 1994.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Frederik de Klerk alifariki, Novemba 11, 2021, akiwa na umri wa miaka 85.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Frederik de Klerk alifariki, Novemba 11, 2021, akiwa na umri wa miaka 85. © AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Ni wakati wa uongozi wake ambapo Nelson Mandela aliachiwa huru kutoka gerezani na baadaye kuwa rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo mwaka wa 1994.

Rais Ramaphosa amemkumbuka De Klerk kama kiongozi aliyekataa shinikizo za chama chake na kuamua kumaliza uongozi wa kibaguzi.

Frederik Willem De Klerk alikwenda kinyume ya wengi katika chama chake na raia wa Afrika Kusini Wazungu, waliokuwa wamepotoshwa kuwa, iwapo watu weusi wataongaza itakuwa hatari kwa maisha yao, De clerk alikwenda kinyume na misimamo wa vyombo vya usalama na wafuasi sugu waliokuwa tayari kuchukua silaha kuilinda serikali iliyokuwepo.

De Klerk alifariki dunia Novemba 11 akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kusumbuliwa na saratani

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.