Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Miaka 8 baada ya kifo cha Nelson Mandela, familia yake inaishi vipi?

Mnamo Desemba 5, 2013, baba wa demokrasia ya Afrika Kusini aliaga dunia. Nelson Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 kutoka nyumbani kwake Johannesburg. 

Miaka minane baada ya kifo cha Nelson Mandela, familia yake haina ushawishi ambao mtu anaweza kutarajia.
Miaka minane baada ya kifo cha Nelson Mandela, familia yake haina ushawishi ambao mtu anaweza kutarajia. MICHEL CLEMENT, DANIEL JANIN AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Nelson Mandela Madiba ambaye alikuwa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi, mfungwa wa kisiasa, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na rais wa kwanza wa Afrika Kusini baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi, bado anasalia kuwa nguzo na atakumbukwa nchini humo. Wakfu muhimu wa Nelson Mandela bado unafanya kazi. Kwa upande mwingine, familia yake haina ushawishi ambao mtu angetarajia.

Wajukuu 17 wa Nelson Mandela wanaishi kwenye kivuli cha Colossus. Baada ya kifo cha Madiba, warithi wake badala yake walijaribu kutengeneza njia yao wenyewe.

Hakuna nasaba ya Mandela katika siasa za Afrika Kusini. Baada ya Nelson, rais, kulikuwa na Zindzi Mandela, mwanadiplomasia binti aliyefariki mwaka 2020. Kisha, leo, Mandla, mjukuu na mbunge wa chama cha ANC. Ni kidogo kwa jina la kifahari kama hilo. Katika familia, siasa ni sawa na mateso, anaeleza Ndileka, mjukuu wa kwanza wa Nelson Mandela.

"Watu hawaelewi ilikuwaje kwa mababu zangu kujitolea kutetea uhuru wa mtu mweusi na demokrasia. Matokeo yake ni kwamba hatuna tena hamu na siasa, "amesema.

Kuanzia kwenye siasa, wajukuu wa Mandela wamejihusisha na masuala ya kibinadamu, fasihi na ujasiriamali. Hiki ndicho kisa cha Tukwini aliyeanzisha mradi uitwao "Jumba la Mandela" akiwa na mamake mwaka 2010. Duka la sanaa linalouza mvinyo, vito vya thamani au nguo na ambalo linataka kusimulia hadithi ya ukoo badala ya mtu binafsi, amebaini Tukwini.

"Tulitaka kwanza kutoa heshima kwa mababu zetu. Kisha tulitaka kusimulia hadithi halisi ya Jumba la Mandela, lakini watu wanaonekana kuamini kwamba babu yangu alikuja kutoka mbinguni kama mmoja wa miungu inayoabudiwa, jambo ambalo si kweli ”, ameongeza.

Leo, familia imetawanyika. Baada ya tukio la kifo cha Nelson Mandela mwaka 2013 na ugomvi wa mirathi uliofuata, sasa kila mtu anafuata njia yake bila kujaribu kufuata nyayo za baba wa demokrasia ya Afrika Kusin.

Maandamano ya kupinga ufisadi, kwa ajili ya kumuenzi Nelson Mandela yalikuwa yafanyike Jumapili asubuhi huko Pretoria, lakini yalifutwa kutokana na kuzorota kwa kasi kwa hali ya afya nchini Afrika Kusini. kirusi kipya cha Omicron kinaenea kwa kasi nchini Afrika Kusini. Kufikia Ijumaa jioni, viongozi waligundua kesi mpya 16,000 za maambukizi ya kirusi hicho katika kipindi cha saa 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.