Pata taarifa kuu

IMF kuipa Zambia dola bilioni 1.4

Zambia ambayo ni nchi ya kwanza barani Afrika kutolipa deni lake baada ya kuanza kwa janga la Covid-19, inaona sasa maendeleo baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, kukubali kutoa mkopo wa dola bilioni 1.4 kwa miaka mitatu.

Rais Hakainde Hichilema mjini Lusaka, Agosti 16, 2021.
Rais Hakainde Hichilema mjini Lusaka, Agosti 16, 2021. © Tsvangirayi Mukwazhi/AP
Matangazo ya kibiashara

Kuingia madarakani Agosti mwaka jana kwa rais mpya, Hakainde Hichilema, na nia yake ya kurekebisha mfumo wa mtangulizi wake, inaonekana, umeishawishi IMF kuunga mkono Zambia.

Alipoingia madarakani mwezi Agosti mwaka jana, Hakainde Hichilema aliahidi kutoa mwanga juu ya deni lililolimbikizwa na utawala uliopita wa Edgar Lungu. Katika miaka sita, Zambia ilikuwa imeona deni lake likiongezeka mara saba, na kukusanya mzigo unaokadiriwa kuwa karibu dola bilioni kumi na tatu za deni, sehemu kubwa ikiwa na China. Yote katika hali isio ya uwazi kabisa na bila Bunge au raia kujulishwa.

Tangu mwezi Septemba, rais Hichilema ameanza mazungumzo na IMF juu ya mageuzi yatakayofanywa na juu ya kuanzishwa kwa mpango wa kupanga upya.

Mwezi Oktoba, IMF ilikaribisha rasimu ya bajeti yake, nia yake katika mageuzi ya kodi na kupunguza matumizi ya umma. Mafanikio haya yamewezesha utoaji wa mkopo wa dola bilioni 1.4 kwa miaka mitatu. Ukweli unabakia kuwa kama mamlaka ya Zambia imekomesha usimamizi mbovu na rushwa katika ngazi ya juu ya serikali, athari ya mfumo wa utawala wa m wake, ambazo zilianza kuonekana baadaye tena kwa muda mrefu. Hakika, ili kushawishi IMF, rais mpya alipendekeza kuondoa ruzuku kwa mbolea, umeme na mafuta, ambayo inaweza kusababisha raias kupandwa na hasira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.