Pata taarifa kuu

Afrika Magharibi: Operesheni dhidi ya ugaidi yawezesha kukamatwa washukiwa 300

Nchini Burkina Faso, mamlaka inatathmini operesheni ya pamoja ya kijeshi kati ya Burkina Faso, Côte d'Ivoire, Togo na Ghana ambayo ilifanyika kuanzia Novemba 21 hadi 27.

Wanajeshi wa Burkina Faso.
Wanajeshi wa Burkina Faso. © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa siku tano, karibu askari 5,720 walishika doria kwenye maeneo ya mipaka yao ya pamoja. Operesheni hiyo iliyoitwa "Koudanlgou 4 zone 2" ambayo ilipangwa na kuzinduliwa nchini Burkina Faso,  iliwezesha kukamatwa washukiwa 300 katika muktadha wa mapambano dhidi ya kuendelea kwa hali ya kigaidi na vitisho kwa usalama wa kitaifa wa nchi wanachama wa "Initiative d'Accra".

Vikosi vya Burkina Faso, Côte d'ivoire, Togo na Ghana viliwakamata washukiwa 300, wakiwemo watu wanaosakwa na vyombo vya usalama. Silaha na risasi kadhaa pia zilikamatwa.

“Shughuli hizi za ulinzi na usalama ziliwezesha kuwakamata watuhumiwa zaidi ya 300 ambao wengi wao walikuwa wanatafutwa na vyombo vyetu vya upelelezi, na kukamata silaha 53 na risasi nyingi, kiasi kikubwa cha vilipuzi na baruti, magari 144, ikiwa ni pamoja na pikipiki," amesema Maxime Koné, Waziri wa Usalama wa Burkina Faso.

Nchini Burkina Faso, operesheni hii ya Koudanlgou 4 ilihusisha maeneo ya maporomoko ya maji, kusini-magharibi, katikati-mashariki, katikati-kusini na katikati-magharibi. Kutoka mikoa ya mpaka ya Côte d'Ivoire, Ghana na Togo. Vituo vitano vya magaidi viliharibiwa, na karibu magaidi thelathini waliuawa wakati wa mapigano, kulingana na Waziri wa Usalama.

Vikosi vya ulinzi na usalama vya Burkina Faso, Togo, Ghana na Côte d'Ivoire viliharibu mashamba ya dawa za kulevya na kutegua vilipuzi vilivyokuwa vimetegwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.