Pata taarifa kuu

Nge washambulia watu na kusababisha vifo kadhaa Misri

Raia nchini Misri katika baadhi ya maeneo wamevamiwa na nge na kusababisha vifo baada ya dhoruba za mvua na mchanga kufukua makundi ya nge wenye sumu na kuwashambulia raia. Watu watatu walifariki dunia baada ya kuumwa na nge wenye sumu na takriban 400 wamejeruhiwa kusini mwa nchi

Kanisa kuu la Coptic huko Aswan  likionekana kutoka Mto Nile, Misri.
Kanisa kuu la Coptic huko Aswan likionekana kutoka Mto Nile, Misri. Michel Benoist/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Kawaida mvua kubwa ikinyesha nge husombwa kutoka kweye maficho yao na kuzagaa mtaani kama ilivyo kwa nyoka, ambao pia husombwa na maji kutoka kwenye mashimo yao.

Hospitali na vituo vya matibabu vya Aswan vimejaa wagonjwa walioumwa na nge hao wenye sumu. Mji wa Aswan kusini mwa Misri ndio ulioathirika zaidi na uvamizi wa nge hao, ambapo mvua kubwa ya mawe pamoja na radi katika eneo karibu na Mto Nile ilishuhudiwa siku ya Ijumaa.

Watu wamehimizwa kupunguza kutembea mitaani na kukaa kwa tahadhari majumbani pamoja na kuepuka maeneo yenye miti mingi.

Gavana wa Aswan, Ashraf Attia, ametangaza masharti ya watu kusafiri katika mji huo kutokana na hali ya hewa ya mvua kubwa na ukungu unaosababisha madereva kutoona vizuri.

Mamlaka nchini humo zimechukua hatua ambapo mpaka sasa dozi za ziada za kuzuia sumu zimetolewa kwa vituo vya matibabu katika vijiji vilivyo karibu na milima na jangwa, afisa wa afya aliliambia shirika la habari la Al-Ahram

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.