Pata taarifa kuu
ETHIIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Waasi wa Tigray wapiga kambi kwenye lango la mji wa Dessie

Jeshi la Ethiopia lilitekeleza shambulizi ya angaa katika mji mkuu wa jilbo la Tigray la Mekele, na kusababisha vifo vya watu 10 kwa mujibu wa hospitali moja katika mkoa huo.

Mmoja wa wanamgambo wa Amhara akiwa akitoa ulinzi katika mji wa Dessia, Ethiopia.
Mmoja wa wanamgambo wa Amhara akiwa akitoa ulinzi katika mji wa Dessia, Ethiopia. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Shirikisho limefanya mashambulio haya huku wakati huo huo likionekana kushindwa katika eneo la kusini, katika eneo la Amhara. Mji wa Dessie uko karibu kuzingirwa. Na sasa vita vinanukia na vinaweza kuwa vyenye maamuzi katika muendelezo wa vita hivi ambavyo vimedumu kwa karibu mwaka mzima.

Serikali jijini Addis Ababa imethibitisha kutekeleza shambulizi hilo kwa kile inachosema, ni kulenga kampuni, inayotumiwa na waasi wa Tigray.

Afisa wa hospitali na vyanzo kutoka upande wa waasi vimethibitisha shambulio hilo na kudai kuwa limewaua watu sita na kuwajeruhi wengine 21.

 Mawasiliano yamekatwa katika sehemu kubwa ya eneo la Kaskazini mwa Ethiopia na waandishi wa habari wamezuiwa na hivyo kufanya taarifa hizo kuwa ngumu kuthibitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.