Pata taarifa kuu
SUDAN-UCHUMI

Sudan yaminywa kifedha, maandamlano yaendelea

Nchini Sudan, waandamanaji wameendelea kujitokeza kupinga hatua ya jeshi kuchukua madaraka wiki hii, huku mashirika mbalimbali ya jumuiya ya Kimataifa kama Benki ya Dunia yakichukua hatua dhidi ya uongozi wa kijeshi.

Mitambo iliyoweka kwenye bandari huko Port Sudan, Oktoba 2021.
Mitambo iliyoweka kwenye bandari huko Port Sudan, Oktoba 2021. © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Benki ya dunia imetangaza kusitisha kutoa msaada wa fedha kwa Sudan, kufuatia hatua hiyo ya jeshi kuchukua madaraka kutoka kwa serikali ya kiraia.

Hatua hii ya Benki ya dunia, inarudisha nyuma hatua ambazo nchi hiyo ilikuwa imeanza kupiga kiuchumu, na inarejesha kutengwa kwa Sudan kushirikiana na taasisi za kimataifa za fedha kama ilivyokuwa wakati wa uongozi wa kiongozi wa zamani Omar Al Bashir na ni mwezi Machi tu, iliruhusu Sudan kupata Dola Bilioni Mbili.

Marekani nayo wiki hi, ilitangaza kusitisha msaada wake wa kifedha wa Dola Milioni 700.

Siku ya Jumatano,  Umoja wa Afrika não umetangaza kuisimamisha Sudan kama mwanachama wake, kwa kile Umoja huo inachosema hatua zilizochukuliwa na jeshi ni kinyume cha Katiba.

Wakati hayo yakijiri, waandamanaji wameendelea kujitokeza jijini Khartoum kupinga hatua ya jeshi kuchukua madaraka.

Jeshi ambalo limevunja serikali ya mpito, limejitetea kwa uamuzi wake, kwa kile ambacho inasema ulilelenga kuzuia umwagaji damu, kufuatia maandamano ya wananchi katika siku zilizopita kuhusu uongozi wa kiraia.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanasema, huo ulikuwa mpango wa jeshi wa kutaka kuendelea kutawala Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.