Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HAKI

Shahidi wa kwanza katika kesi ya mauaji ya Thomas Sankara atoa ushuhuda

Nchini Burkina Faso, kesi ya mauaji ya mwanamapnduzi mashuhuri Thomas Sankara aliyeuawa kwa kupigwa risasi nchini humo miaka 34 iliyopita inaendelea kusikilizwa kwa siku ya tatu mfululizo, kuanzia Jumatatu wiki hii ilipofunguliwa.

Watu wakihudhuria ufunguzi wa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya Thomas Sankara huko Ouagadougou Oktoba 11, 2021
Watu wakihudhuria ufunguzi wa kesi ya washtumiwa wa mauaji ya Thomas Sankara huko Ouagadougou Oktoba 11, 2021 AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Shuhuda wa kwanza, Elisée Ilboudo aliyekuwa mwanajeshi wakati kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Thomas Sankara, alipouwa  miaka 34 iliyopita,  anaendelea kushuhudia kuhusu namna mauaji hayo yalivyotekelezwa.

Siku ya Jummane, alibaini kwamba makomando wa waliokuwa wanamlinda Blaise Compaoré waliwasili kwneye eneo alilokuwa Snakara na kumpiga risasi.

Mariam Sankara, mkewe Thomas Sankara anafuatila kwa karibu kesi hiyo kwenye Mahakama ya kijeshi jijini Ouagadougou.

Utata juu ya kifo chake

Ukweli kamili haujabainika kuhusu mazingira na wale waliohusika kwa kifo chake wakati wa mapinduzi ya mwaka wa 1987. Mjane wake Mariam Sankara bado anatafuta haki. Vipimo vya vinasaba – DNA vilifanywa kwa mabaki yanayodaiwa kuwa ya kiongozi huyo wa Burkina, lakini havikuwa kamilifu. Waranti wa kimataifa wa kukakamatwa umetolewa dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaoré, anayeishi sasa uhamishoni. Kuna miito mingi kwa Ufaransa kutoa ruhusa ya kuchunguzwa nyaraka zake za zamani kuona kama koloni hilo la zamani lilihusika na kifo cha “Che Guevara wa Afrika”.

Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré, akiweka shada la maua kwenye miguu ya sanamu ya mwanamapinduzi mashuhuri Thomas Sankara aliyeuawa na kundi la makomando.
Rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré, akiweka shada la maua kwenye miguu ya sanamu ya mwanamapinduzi mashuhuri Thomas Sankara aliyeuawa na kundi la makomando. AFP - OLYMPIA DE MAISMONT

Kiongozi wa mapinduzi Thomas Sankara anazingatiwa kuwa mmoja wa vigogo wa kisiasa barani Afrika wa karne ya 20, pamoja na Patrice Lumumba na Nelson Mandela

Maisha ya Thomas Sankara

Kapteni Thomas Sankara, aliezaliwa mwaka 1949, alichukua madaraka wakati wa mapinduzi ya Agosti 4 1983. Akiwa na mshirika wake jeshini, akaipa Upper Volta, kama ilivyoitwa na mkoloni wake Ufaransa, jina la Jamhuri ya Kidemokrasia na Maarufu ya Burkina Faso, ambalo lina maana “nchi ya watu waaminifu”. Akatolewa madarakani na mmoja wa marafiki zake, Blaise Compaoré, kisha akauliwa mnamo October 15, 1987 pamoja na wenzake 12.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.