Pata taarifa kuu
ESWATINI-USALAMA

Ujumbe wa SADC ziarani Eswatini baada ya maandamano yaliyosababisha vifo vya watu 7

Ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na waziri wa zamani wa Afrika Kusini, unatarajia kukutana na Mfalme Mswati III nchini Eswatini, baada ya maandamano mabaya katika siku za hivi karibuni.

Maandamano mapya huko Mbabane yalisababisha vifo vya watu saba Oktoba 20, 2021, huko Eswatini.
Maandamano mapya huko Mbabane yalisababisha vifo vya watu saba Oktoba 20, 2021, huko Eswatini. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashirika ya kiraia, angalau watu saba waliuawa Jumatano hii, Oktoba 20, 2021 wakati wa maandamano dhidi ya serikali hiyo.

Maandamano hayo, yaliyoitishwa na wafanyakazi, yalidhinishwa na mamlaka kabla ya kupigwa marufuku. Siku ya Jumatano, polisi na jeshi walijaribu kuzuia na kutawanya waandamanaji mia kadhaa ambao walikuwa wakijaribu kukusanyika katika mji mkuu wa Mbabane.

Siku ya Jumatano jioni, chama cha wafanyakazi ulisemamtu mmoja aliuawa na angalau 80 walijeruhiwa. Alhamisi hii asubuhi, mashirika ya kiraia yalibaini kwamba watu saba ndio waliouawa, takwimu ambayo bado haijathibitishwa. Maandamanoya mwisho mnamo mwezi Mei na Juni 2021 yaliua zaidi ya watu ishirini.

Waandamanaji wanataka demokrasia zaidi katika nchi hii ya utawala wa kifalme, ambapo waziri mkuu anachaguliwa na mfalme na vyama vya kisiasa vimepigwa marufuku kwa zaidi ya miaka 40.

Waandamanaji kwa hivyo wanataka mabadiliko katika Katiba, uhuru zaidi wa kisiasa, uhuru wa kujieleza. Wanataka pia kuachiliwa kwa wabunge wawili, wanaozuiliwa tangu mezi Julai, ambao walishtakiwa kwa uhaini na mauaji baada ya kutaka mageuzi na kuunga mkono harakati za maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.