Pata taarifa kuu
ESWATINI - USALAMA - SIASA

Serikali ya Eswatini yakanusha taarifa za Mfalme Mswati III kukimbia nchi

Serikali ya Eswatini, imekanusha taarifa za Mfalme Mswati III, kulimbia taifa hilo la kusini mwa Africa kufuatia makabiliano ya wanajeshi na wandamanaji wanaoshikiza mageuzi nchini humo.

Mfalme  Mswati III, wa Eswatini
Mfalme Mswati III, wa Eswatini AFP/File
Matangazo ya kibiashara
Ningependa kuwahakikishia raia wa eswatini na jamii ya kimataifa kuwa Mfalme Mswati II yupo nchini na anaendelea na majukumu yake ya kujenga ufalme wa Eswatini 

taarifa kutoka kwa kaimu waziri mkuu Themba Masuku, imesema.

Masuku ametoa wito wa utulivu kipindi hiki cha maandamano.

Maandamano dhidi ya mfulme Mswati III, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 yalianza wikendi iliopita wandamanaji wakishinikiza mabadiliko ya katiba na kuondoka madarakani kwa Mswati III, kama njia ya kuelekea kwa demokrasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.